Pages


Home » » WAHAMIAJI HARAMU WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.

WAHAMIAJI HARAMU WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.

Kamanga na Matukio | 01:40 | 0 comments

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbozi.
Raia 7 wa nchi ya Somalia na mmoja wa nchi ya Kenya wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mbozi, Mkoani Mbeya mbele ya Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Rahim Mushi, kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria.

Mwendesha mashtaka wa Jeshi la Polisi Staff Sajent Amin Rajab, ameiambia mahakama hiyo kuwa mnamo Machi 25 mwaka huu raia hao walikamatwa Mji mdogo wa Tunduma na kufikishwa mahakamani Machi 26 mwaka huu.
 
Ameongeza kuwa kesi hiyo namba 56, raia hao wamefanya kosa hilo kinyume cha sheria kifungu cha 31:1(i) na kifungu cha 2 cha sheria ya uhamiaji ya mwaka 1995, ambapo amewataja wahamiaji hao kuwa ni pamoja na Salad Yusuph(20), Abdillah Abdi(20), Mohammed Idd Hussein(20), Mohammed Ahmed Abdi(13) na Ahmed Athuman(22).

Wengine ni Abdirizack Abdlahaman(19), Nuru Yusuph Ally (35) wote ni wakazi wa Mogadishu nchini Somalia na Ibrahim Ally(30), mkazi wa Nairobi nchini Kenya.

Hata hivyo kesi hiyo itatajwa tena April 10 mwaka huu na washtakiwa wapo mahabusu .
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger