Zoezi la kupima magonjwa ya Kisukari, shinikizo la damu na unene ambapo vipimo hivyo hutolewa bure na wataalamu wa afya kutoka AFPTA katika viwanja vya Ruanda Nzovwe jijini Mbeya.
Mgeni rasmi Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa Luis Choboko, akihutubia wananchi waliojitokeza katika zoezi la kupima magonjwa ya Kisukari, shinikizo la damu na unene ambapo vipimo hivyo hutolewa bure na wataalamu wa afya kutoka AFPTA katika viwanja vya Ruanda Nzovwe jijini Mbeya.
Zoezi la kupima magonjwa hayo, katika Wilaya ya Mbozi mkoani hapa.
Mgeni rasmi Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa Luis Choboko, akipima magonjwa ya Kisukari, shinikizo la damu na unene ambapo vipimo hivyo hutolewa bure na wataalamu wa afya kutoka AFPTA katika viwanja vya Ruanda Nzovwe jijini Mbeya.
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mamia ya wakazi wa jiji la Mbeya wamejitokeza jana katika viwanja vya Ruanda Nzovwe kwa ajili ya kupima magonjwa ya Kisukari, shinikizo la damu na unene ambapo vipimo hivyo hutolewa bure na wataalamu wa afya kutoka AFPTA.
Akifungua zoezi hilo Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa Luis Choboko amesema zoezi hilo linamanufaa makubwa kwa wananchi ambapo ametoa wito kwa jamii kujitokeza kwa wingi kupima afya zao.
Amesema zoezi hilo limelenga kupunguza msongamano wa watu kwenye vituo vya afya ambao huenda kwa ajili ya kupima zao na kwamba zaoezi hilo linatarajiwa kumalizika kesho.
Zoezi la upimaji wa afya katika viwanja vya shule ya Msingi Ruanda Nzovwe linakwenda sambamba na utoaji wa elimu ya mwananchi kujiunga na mifuko ya jamii.
Hata hivyo zoezi hili lilianzia wilaya ya Mbozi na kupata mafanikio makubwa, na kwamba zoezi litamalizika Machi 18 mwaka huu Jijini Mbeya na kuendelea katika mikoa ya Mwanza na Arusha.
0 comments:
Post a Comment