Mgeni Rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bi. Betha Swai akiwahutubia wanawake pamoja na wananchi walio fika katika Sherehe za kuazimisha siku ya wanawake Duniani Jijini Mbeya, katika viwanja vya Luanda Nzovwe.
Afisa Maendeleo Jamii Mkoa wa Mbeya Bi. Stella Kategile akisoma risala ya kuazimisha siku ya wanawake Duniani jijini Mbeya.
Mwenyekiti wa Sherehe hizo Bi.Mary Tolemi akitoa Taarifa kwa Mgeni Rasmi .
Katibu tawala mkoa wa Mbeya Beatha Swai amewataka wanawake kufanya kazi kwa bidii ili waweze kuondokana na wimbi la umasikini ambalo limekuwa likiwakabilia hasa wanawake.
Ameyasema hayo leo kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo yameadhimishwa kiwilaya katika viwanja vya shule ya Msingi Ruanda Nzovwe huku kauli mbiu ya maadhimisho hayo ikiwa ni USHIRIKI WA MSICHANA UNACHOCHEA MAENDELEO”
Wakati huohuo Bi.Swai alitoa zawadi kwa wanafunzi watatu waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha nne mwaka 2011 ambao ni Feliste Silivesta kutoka Mbeya Sekondari, Jacklini Hindi kutoka Samora Sekondari na Grace Mikola kutoka Mbeya Sekondari.
Naye mwenyekiti wa kamati ya maadhimisho hayo Bi.Mery Gumbo amewataka wanawake kuwa wepesi kushirikiana kwa kujiunga kwenye vikundi vitakavyowawezesha kujipatia kipato.
0 comments:
Post a Comment