Pages


Home » » MAKUNDI YAENDELEA KUIMALIZA CHADEMA MKOANI MBEYA.

MAKUNDI YAENDELEA KUIMALIZA CHADEMA MKOANI MBEYA.

Kamanga na Matukio | 05:41 | 0 comments
Habari na Angelica Sullusi, Mbeya.
Makundi  ya Uchaguzi  mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ngazi ya Taifa wa mwaka 2009 yamedaiwa kukivuruga chama hicho Mkoani Mbeya na kusababisha baadhi ya viongozi kujiuzulu.

Wakizungumza na waandishi wa habari baadhi ya viongozi na Wanachama wa Chadema Mkoani hapa wamesema kuwa hali ya chama hicho mkoani hapa kwa sasa siyo nzuri hivyo kusababisha baadhi ya viongozi kukata tamaa kuendelea na nyazifa zao za uongozi.

Mmoja wa Viongozi waanzilishi wa chama hicho Mkoani hapa George Mtasha amesema kuwa mchakato wa kuwaondoa madarakani viongozi wanaodaiwa kumuunga mkono Zitto kipindi kile cha mchakato wa uchaguzi 2009 umeanza Januari 11, mwaka hu katika mkutano wa baraza la Mashauriano la Mkoa uliofanyika katika ukumbi wa hotel ya Mount Livingstone Jijini hapa.

 Mtasha amesema kuwa  katika kikao hicho kilichoongozwa na Dk. Wilbroad Slaa, uongozi Mkoa uliagizwa kufanya kama alivyofanya yeye  baada ya kuvunja uongozi wa Mkoa uliokuwepo kwa madai ya  kusafisha chama.

Amesema kuwa baada ya kubaini kuwa  kuna mizengwe inayofanywa kwa lengo la kuwaondoa madarakani baadhi ya watu ndipo alipoamua kujihudhuru February  10,2012 wadhifa huo.

Kwa upande wake aliyekuwa Katibu  wa Chadema Mkoa wa Mbeya Eddo Makatta amesema kuwa kuondolewa kwake katika wadhifa ni kutokana na kile kilichodaiwa kuwa  yupo upande wa Zitto.

Aidha, viongozi hao wamesema kuwa pamoja na kuwepo kwa makundi hayo bado wataendelea kukililia chama chao kwa kuhakikisha kinashika dola kwa kuwa wanachama na wakereketwa wa chama hicho.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger