Pages


Home » » APRM YAFANYA SEMINA YA SIKU MOJA MKOANI MBEYA.

APRM YAFANYA SEMINA YA SIKU MOJA MKOANI MBEYA.

Kamanga na Matukio | 04:23 | 0 comments

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Asasi isiyo ya Kiserikali barani Afrika inayojulikana kama Mpango wa hiari wa kujitathimini, Utawala bora kwa nchi za hilo (APRM), imefanya semina ya siku moja katika Ukumbi wa Paradise uliopo jijini Mbeya.

Semina hiyo ilifunguliwa na Katibu Mtendaji wa APRM Bi Rehema Twalib.na kujumuisha taasisi mbalimbali za Serikali nchini , wabunge, wanasiasa, asasi zisizo za kiraia, wataalamu wa kada mbalimbali na wanahabari.

Katika Hotuba yake Bi Rehema alisema lengo la semina hiyo ni tathimini katika Utawala bora, uchumi na huduma za kijamii barani Afrika na Tanzania ni miongoni mwa nchi wanachama na Mkoa wa Mbeya ni miongoni mwa mikoa iliyoteuliwa kuwakilisha mawazo kwa niaba ya wakazi wa Nyanda za Juu kusini.

Baadhi ya wajumbe waliohudhuria semina hiyo ni kutoka nchi za Kenya, Zanzibar, Uganda, Rwanda na Afrika Kusini kama Profesa Muhidin kutoka nchi ya Kenya, Profesa Ruth Meena na wabunge Said Amour Alfi na John Shibuda.

Miongoni mwa changamoto zinazoikabili Tanzania ni ukosefu wa maadili katika Taasisi za serikali kama magereza, Polisi, mahakama, ambazo zinaleta msongamano wa kesi na mahabusu ambao hurundikana, hivyo ni kukiuka haki za binadamu.

Pia mifumo mibovu ya elimu, utawala bora na ukosefu wa ajira zimetajwa kuwa ni miongoni mwa sababu vyanzo vya migomo na maandamano nchini.

Baada ya kumaliza kutembelea kanda zote nchini APRM itatoa rasimu yake na kumkabidhi Raisi wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye ataisoma  aua kuiwakilisaha mbele ya Marais wanachama wa asasi hiyo barani Afrika.

Hata hivyo asasi hiyo itakuwa ni wajibu wa kumshauri Rais mapendekezo maoni na ushauri  kama Rais akikaidi atafikishwa mbele ya Marais wenzakekabla hatua nyingine hazijachukuliwa lakini pia Rais atashauriwa endapo kuna mapendekezo yanayoweza kuisaidia Serikali kuondokana na wimbi la umasikini.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger