Habari na Angelicia Sullusi, Mbeya.
Watanzania zaidi ya Milioni kumi na tano wenye uwezo wa kufanya kazi hawana huduma ya mifuko ya hifadhi ya Jamii NSSF kutokana na sababu mbalimbali.
Hayo yamesemwa hivi karibuni na Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF Mkoa wa Mbeya, Hamis Fakii wakati akijibu maswali ya wanachama wa mfuko huo ambao ni walimu wa shule za Jumuiya ya Wazazi wa Mkoa wa Mbeya katika semina ya mafunzo iliyofanyika juzi Jijini Mbeya.
Fakii amesema kuwa kwa takwimu za sensa ya mwaka 2002, zinaonyesha kuwa Tanzania ina jumla ya watu milioni thelathili ambapo wenye uwezo wa kufanya kazi ni watu milioni kumi na sita tu.
Amesema kati ya watu hao ni watu milioni moja tu ndio wanaofanya kazi,na wanaopata huduma za mifuko ya hifadhi ya jamii, kati yao asilimia 53 wamejiunga na NSSF, asilimia 26 wamejiunga na mfuko wa hifadhi ya Jamii wa PSPF na asilimia zilizobaki wamejiunga katika mifuko ya PPF na LAPF.
Fakii amezitaja sababu kadhaa zinazosababisha watu wengi kutojiunga na mifuko ya hifadhi ya Jamii, kuwa ni kutokuwa na ajira rasmi zinazotambulika, kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya faida za kujiunga na mifuko ya hifadhi za jamii, hali ambayo inawafanya wasihamasike kujiunga na kuchangia mifuko hiyo.
0 comments:
Post a Comment