Pages


Home » » CCM KATA YA TUNDUMA WILAYA YA MBOZI YATOA MISAA DA YA MIFUKO YA SARUJI NA MATOFARI - MBEYA

CCM KATA YA TUNDUMA WILAYA YA MBOZI YATOA MISAA DA YA MIFUKO YA SARUJI NA MATOFARI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:18 | 0 comments

Na.Shomi Mtaki, Mbozi 

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Tunduma wilayani Mbozi, kimetoa msaada wa mifuko ya saruji 76 na matofari 2000 kwa ajili ya shule za msingi nane zinazojengwa katika halmashauri ya mji wa Tunduma.

Msaada huo wenye thamani ya sh. Milioni 3.5, unalenga  kuharakisha kukamilisha ujenzi wa madarasa ya shule mpya zinazojengwa kwa nguvu ya wananchi, kwa lengo la kuwanusuru wanafunzi wa darasa la kwanza waliokosa nafasi ya kuanza masomo yao mapema mwaka huu.

Hafla fupi ya kukabidhi msaada huo ilifanyika jana katika ofisi za halmashauri hiyo, ambapo uongozi wa kamati ya siasa chini ya Mwenyekiti wake Danny Mwashiuya, ulimkabidhi ofisa mtendaji wa halmashauri hiyo.
 

Akipokea msaada huo ofisa huyo Aidany Mwanshiga alikipongeza CCM kwa kuonyesha njia ya kusaiodia hatua zinazochukuliwa na halmashauri yake ya kukabiliana na ongezeko kubwa la watoto wanaotarajia kuanza darasa la kwanza mapema mwezi huu.
 
 Alizitaja shule zitakazo nufaika na msaada huo kwa kupata saruji mifuko 10 kila moja kuwa ni Migombani, Maporomoko, Sogea, Majengomapya, Mwaka, Claster, Manga itakabidhiwa mifuko 16 na shule ya Mkombozi itapewa matofari 2000.
 
Mwenyekiti wa alisema, CCM imeguswa na kilio cha wananchi  wanaojitolea kujenga shule hizo lakini kutokana na baadhi ya changamoto zinazowakabili wameshindwa kukamilisha mapema ujenzi huo na kusababisha watoto  hao kuchelewa kuanza masomo yao Januari 9 mwaka huu.
 
Mwashiuya alisema hatua hiyo ni utekerezaji wa Irani na Sera za chama chake kwa kuhakikisha  kila mtoto anayestahili kupata haki zake za msingi anazipata, kwa kuwa huo ndiyo urithi muhimu kwa ajili ya watoto hao..
 
Alisema msaada huo umetolewa baada ya kamati za ujenzi wa shule hizo kuwakilisha maombi katika ofisi zake mapema Januari mwaka huu na kwamba mgao huo umezingatia mahitaji yaliyoombwa.
 
Aidha mwenyekiti huyo alisema CCM itaendelea kutoa misaada ya hali na mali katika jamii kulingana na uwezo wake wa mapato yanayopatikana kupitia vitega uchumi vyake vilinyopo mjini hapa pamoja na michango ya wanachama wake.
 
 Alisema kuna baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanawadanganya wanacnhi kwa kudai kuwa eti CCM hakichangii maendeleo ya jamii,jambo ambalo halina ukweli.
 
”Ukweli ni kwamba CCM kinathamini huduma za kijamii hivyo kitahakikisha kinachangia huduma hizo kadri kinavyoweza kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi wake,’alisema.
 
Kwa upande wake diwani wa kata hiyo Frank Mwakajoka   (Chadema) alisema halmashauri hiyo inathamini msaada huo ambao umetolewa wakati mwafaka na akavitaka vyama vingine vya siasa na taasisi mbalimbali kuiga mfano wa huo.
 
Alisema kitendo hicho kitwafurahisha sana wanacnhi wa Tunduma na kwa mba hiyo itafuta dhana potofu iliyokuwa ikihubiriwa katika majukwa ya kisiasa ya kukipaka matope  chama hicho kuwa kilikuwa kikizuia wananchi wasichangie   maendeleo.
 
“Nawashukru sana viongozi wa CCM kata ya Tunduma kwamba wameamua kuunga mkono ujenzi wa shule za msingi na waendelee kufanya hivyo ili kufuta tafsiri potofu za watu ukweli CCM inaonyesha kuwa inaunga mkono maendeleo ya mji wa Tunduma.
 
Kwa mujibu wa diwani huyo kata hiyo inaupungufu wa madarasa 220 kati ya madarasa 300 yanayohitajika kwa ajili ya wanafunzi 14,144.

Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger