Pages


Home » » WATU 10 WATUHUMIWA KUCHOMA NYUMBA YA MWANAKIJIJI NA KUMTEKA MKEWE

WATU 10 WATUHUMIWA KUCHOMA NYUMBA YA MWANAKIJIJI NA KUMTEKA MKEWE

Kamanga na Matukio | 05:42 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Watu 10 wakazi wa Kijiji cha Bara, Wilaya ya Mbozi Mkoani ambao baadhi yao ni viongozi wa kijiji hicho wamebomoa  nyumba na kuteketeza vitu vilivyokuwemo ndani.

Nyumba hiyo inayomilikiwa na Bwana Jumapili James Mwampamba (40), ilibomolewa Machi 14 mwaka huu majira ya saa 5 asubuhi, watu hao walikimtuhumu mwenye mali hizo kuwa kaiba mbuzi mali ya Juma Mgalla mkazi wa kijiji cha Bara Kati.

Wakati tukio hilo linatokea Bwana Jumapili alikuwa safarini ndipo walipomkosa na kisha kuchukua jukumu la kuvunja mlango na kuteketeza kila kitu kilichokuwemo ndani, vikiwemo vyakula, magodoro, madaftari ya shule, pikipiki aina ya Honda ambayo waliivunja vunja kwa kutumia mashoka.

Aidha watu hao hawakuishia hapo, ambpo walimteka nyara mke wa Bwana Jumapili aitwaye Bi. Saina Mgalla (34) ambapo waliondoka naye na haifahamiki mpaka sasa wapi alipo na katika hali isiyokuwa ya kawaida waliviteketeza kwa moto vidonge ARVs vilivyokuwa vikitumiwa na mwanamke huyo.

Hata hivyo watuhumiwa wa tukio hili ni pamoja na Mwenyekiti wa kijiji cha Bara Bwana Lingson Weja, Afisa mtendaji wa kijiji hicho Bwana Watson Maduguli, Afisa mtendaji wa Kata Bwana Martine Twinzi, Katibu wa Kitongoji Bwana Amos Jackson Mwankonde, Mwenyekiti wa Kitongoji wa Itandula Bwana Miliki Julius, Mjumbe wa Kijiji Julius Halinga, Fwanje Juma Mgalla, Ziora Biashara na Juma Mgalla.

Watuhumiwa hao mpaka sasa hawajakamatwa licha ya kufungua jalada lililofunguliwa na mtoto wa Jumapili Mwampamba anayesoma kidato cha tatu shule ya sekondari Bara yenye namba ITK/RB/30/2012, ya Machi 15 mwaka huu katika kituo cha Jeshi la Polisi Itaka.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa matukio hayo na kwamba anafanya uchunguzi na watuhumiwa watukio hilo, watafikishwa mahakamani kujibu shtaka linalowakabili.

Wakati huohuo Bwana Jumapili ameendelea kuishi uhamishoni kutokana na hofu ya kuawa na anaendelea kumtafuta mkewe ili kufahamu alipo na viongozi hao wameendelea kuapa kuwa mtu yeyote atakayefuatilia suala hili atauawa.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger