Pages


Home » » SOKO JINGINE LATEKETEA KWA MOTO MJI MDOGO WA TUNDUMA USIKU WA KUAMKIA LEO.

SOKO JINGINE LATEKETEA KWA MOTO MJI MDOGO WA TUNDUMA USIKU WA KUAMKIA LEO.

Kamanga na Matukio | 05:25 | 0 comments

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Zaidi ya vibanda 7 vya wafanyabiashara katika soko la Black lililopo mji mdogo wa Tunduma wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya  vimeteketea kwa moto kuanzia majira ya saa nane za usiku ambapo chanzo cha moto huo hakijaweza kufahamika.

Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu Mkuu wa wilaya ya hiyo Bwana Gabriel Kimoro amesema kuwa ni zaidi ya vibanda saba vimeteketea kwa moto, ambapo baadhi ya bidhaa zimeokolewa na hali ya ulinzi na usalama na bidhaa hizo umeimarishwa na kwamba  zoezi la udhibiti wa moto unaendelea kwani mpaka sasa wamepata gari la nzima moto kutoka nchi ya jirani ya Zambia na gari jingine linaelekea eneo la tukio kutokea jijini Mbeya.

Hata hivyo hakuna mtu yeyote aliyetajwa kujeruhiwa kutokana na moto huo na hasara iliyopatikana katika ajali hiyo haijaweza kufahamika mara moja.

Mwishoni mwa mwaka jana soko jingine liliungua na kuleta hasara kubwa kwa wafanyabiashara katika mji mdogo huo wa Tunduma na kufunguliwa rasmi na mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta Mohammed Gharib Bilal wiki mbili zilizopita.
*****(Picha na Habari endelea kutembelea mtandao huu)*******
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger