Habari na Ezekiel Kamanga, Mbozi.
Afisa mtendaji wa Kijiji cha Halungu, Wilaya ya Mbozi, Mkoani Mbeya aliyefahamika kwa jina moja la Mkoma, ametoroka baada ya Solar ya umeme wa jua iliyotolewa na Wizara ya Ardhi kwa ajili ya kutengenezea hati za kimila kwa ajili ya kumiliki ardhi kijijini.
Mradi huo uliozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta Jakaya Mrisho Kikwete mwaka 2010, umejikuta ukikwama kutokana na kuibiwa kwa solar hiyo ambayo ilikuwa na uwezo wa kuendesha kompyuta iliyokuwa ikitunza nyaraka za hati za kijiji cha Halungu na Ipunga wilaya ya Mbozi, ambavyo vilikuwa mfano Mkoani hapa na chini kwa ujumla.
Naye, Diwani wa Kata ya Halungu Mheshimiwa Samson Simkoko amesema kupotea kwa solar hiyo ni pigo kubwa kwa Kijiji na Kata yake kwa ujumla kutokana na masjala hiyo kusaidia wananchi kupata hati za ardhi kijijini hapo badala ya kufuatilia Mkoani na Wizarani.
Ameongeza kuwa dada ya solar hiyo kuibiwa Halmashauri ya Wilaya hiyo iliamua kuchukua kompyuta iliyokuwepo kijijini hapo na kuipeleka katika ofisi za Halmashauri na hivyo kwa sasa hakutakuwa na shughuli za upimaji na umilikishwaji wa ardhi kwa njia ya kimila hivyo kuleta usumbufu kwa wananchi.
Diwani Simkoko amesema baadhi ya wananchi walianza kupata manufaa kwenye Asasi za fedha ambazo zimekuwa zikizikubali hati hizo kwa ajili ya mikopo.
0 comments:
Post a Comment