Pages


Home » » HAKIMU ADAIWA KUVUNJA NDOA ZA WATU.

HAKIMU ADAIWA KUVUNJA NDOA ZA WATU.

Kamanga na Matukio | 04:09 | 0 comments

Hii ni barua ambayo Joyce Kapushi alipewa barua ya kwenda kupumzika kwa baba yake aitwaye Saidi Kapushi, kwa muda usiojulikana bila ya mumewe kuitwa mahakamani au katika baraza lolote la usuluhishi la kata au mtendaji hata viongozi wa dini ili kujadili lolote kuhusu wanandoa hao.
 ******
 Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Hakimu Mfawidhi wa mahakama ya mwanzo Mlowo, wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya jina linahifadhiwa anadaiwa kuvunja ndoa za watu kwa kutoa barua za mapumziko kwa wanandoa bila hata kusikiliza mashauri yao mahakamani.

Hayo yamebainishwa na mwandishi wa mtandao huu ambapo baadhi ya barua amefanikiwa kuzipata, ambazo zimekuwa zikiandikwa na makarani wa mahakama hiyo na hakimu huyo kuweka saini yake katika barua hizo.

Hakimu huyo ameufanya mradi endelevu kwa wanawake ambao humpatia pesa kupitia makarani wake ambapo wanawake wamekuwa wakishinikiza wapewe barua za kwenda mapumziko kwa wazazi wao kwa muda usiojulikana.

Tukio hilo ni la hivi karibuni ambapo mwanamke Joyce Kapushi alipewa barua ya kwenda kupumzika kwa baba yake aitwaye Saidi Kapushi, kwa muda usiojulikana bila ya mumewe kuitwa mahakamani au katika baraza lolote la usuluhishi la kata au mtendaji hata viongozi wa dini ili kujadili lolote kuhusu wanandoa hao.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wetu umebaini kuwa zaidi ya barua saba zimeandikwa na hakimu huyo kwa kipindi cha miezi mitatu, huku wanaume wakiishi katika mateso kutokana na manyanyaso ya wanawake hao wakishirikiana na hakimu huyo ambaye hupendelea kutembelea gari ya rangi nyekundu aina ya Suzuki.

Mtandao huu unauliza asasi za wanawake ziko wapi, kuwatetea wanaume hao dhidi ya vitendo vya unyanyasaji?.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger