Pages


Home » » KUFUATIA KIFO CHA MWANAFUNZI WA CHUO CHA TEKU, MZAZI ATAKA FIDIA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA.

KUFUATIA KIFO CHA MWANAFUNZI WA CHUO CHA TEKU, MZAZI ATAKA FIDIA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA.

Kamanga na Matukio | 04:20 | 0 comments
 Baadhi ya majeraha yaliyotokana na kipigo atika mwili wa marehemu Daniel  Godluck Mwakyusa (31) ambaye ni mwanafunzi wa chuo hicho  aliuawa na Askari wa Jeshi la Polisi Februari 14, mwaka huu katika sikukuu  ya wapendanao {valentine day].
******
 Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Baba mzazi wa aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU), anayedaiwa kuawa na askari wa Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya Februari 14 kuamkia Februari 15, mwaka huu Bwana Hezron Mwakyusa ametaka kulipwa fidia kutokana na  kifo cha mwanae marehemu Daniel Mwakyusa .

Baba wa marehemu ameandika barua kupitia mwanasheria wake MWAKOLO AND COMPANY, ADVOCATES, NOTARY, PUBLIC AND COMMISSIONERS FOR OATHS wa jijini Mbeya Februari 25, mwaka huu na mtandao huu kubahatika kuiona nakala kwenda kwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na Mwenyekiti wa haki za binadamu.

Katika barua hiyo kwenda kwa Mwanasheria mkuu wa Serikali mfawidhi, Ofisi ya Mwanasheria mkuu wa serikali mkoa wa Mbeya, Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi na Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoa huu (RPC), Mwakyusa ametaka taarifa ya siku 90 kwa nia ya kufungua shauri na madai ya Shilingi milioni 900 fedha za kitanzania.

Baba wa marehemu mnamo Februari 14, mwaka huu Polisi walikwenda Uyole Universal Pub na askari wa doria walipofika pale, mmoja wao (Jina linahifadhiwa) alimkamata marehemu na kufungua mkanda wa bunduki na kuanda kumpiga kwa kutumia mkanda huo na kisha aliommba askari wenzake wamkamate marehemu na kumpiakia kwenye gari ya polisi na kumpeleka kusikojulikana.

Hata hivyo Februari 16, mwaka huu ndugu wa marehemu walisikia minong’ono juu ya kuuawa kwa ndugu yao, ndipo walipochukua jukumu la kwenda Chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa iliyopo jijini Mbeya na kumtambua marehemu kuwa ni mtoto wao.

Bwana Mwakyuas amesema marehemu alikuwa na majeraha ya risasi, mkono wa kulia jeraha moja na kushoto majeraha mawili na jeraha jingine liliingilia mkono wa kulia na kutokea mkono wa kushoto, kwa muonekano huo mzazi huyo anawatuhumu polisi walihusika kumkamata mtoto wake na kuhusika na kifo chake.

Wakati huohuo mzazi huyo amefuatilia apewe taarifa ya uchunguzi wa daktari (POST MOTERM REPORT), na kukataliwa hali ambayo ameitafsiri kuwa ananyimwa haki zake za msingi ili ufanyiwe uchunguzi wa kisheria na kuchukuliwa hatua zifuatazo:-
(i)               Askari waliohusika na tukio hilo wakamatwe na kushitakiwa kwa mujibu wa sheria,
(ii)            Kupewa taarifa za uchunguzi wa kifo cha mwanawe (POST MOTERM REPORT),
(iii)          Polisi wakanushe kwenye vyombo vya habari taarifa ambayo waliitoa kuwa mwanawe ni jambazi sugu.

Barua ya Bwana Mwakyusa imelitaka Jeshi la Polisi kulipa fidia ya shilingi milioni 900 ndani ya siku 90, kabla ya kufungua madai ya mahakamani.

Mbali na hayo ameongeza kwa kulishukuru Jeshi la Polisi kwa kutoa jeneza na usafiri katika mazishi ya mwanae huyo hadi wilaya ya Kyela.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger