Pages


Home » » WANANCHI WAIKATAA TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI YA KIJIJI CHAO - MBOZI.

WANANCHI WAIKATAA TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI YA KIJIJI CHAO - MBOZI.

Kamanga na Matukio | 01:43 | 0 comments

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbozi.
Wananchi wa Kijiji cha Hampangala, Wilayani ya Mbozi, Mkoani Mbeya wameikataa taarifa ya mapato na matumizi ya kijiji, iliyosomwa na Afisa Mtendaji wa kijiji hicho Bwana Saston Mkondya Februari 24 mwaka huu.

Hata hivyo pamoja na kukataliwa kwa taarifa hiyo Mtendaji huyo aliamua kutengeneza muhtasari wa kugushi na kuupeleka katika ofisi mbalimbali zikiwemo ya diwani na halmashauri ya mji, ambapo alihalalisha mkutano huo ambao ulimalizika kutokana na kukosekana kwa amani.

Aidha baadhi ya wananchi wamesikitishwa na tabia ya Afisa utumishi wa wilaya, baada ya kuendelea kumkingia maovu mtumishi wake, ambaye amekiri kugushi muhtasari hali iliyopelekea wananchi hao kuifunga ofisi hiyo Machi 16 mwaka huu, kufuatia kuchoka na kuchoishwa na vitendo vya mtendaji huyo.

Katika uchunguzi umebaini kuwa kutokana na sakata hilo Mkuu wa wilaya ya hiyo Bwana Gabriel Kimoro, atafanya mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji hicho ili kupata ufumbuzi wa tatizo hilo.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger