Pages


Home » » WATU 7 WAFIKISHWA MAHAKAMANI KUSOMEWA MASHTAKA YANAYOWAKABILI - MBEYA.

WATU 7 WAFIKISHWA MAHAKAMANI KUSOMEWA MASHTAKA YANAYOWAKABILI - MBEYA.

Kamanga na Matukio | 04:03 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Watu saba wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mbozi, mbele ya Hakimu mfawidhi mwandamizi Rahimu Mushi kwa tuhuma za makosa 27 yanayowakabili, yakiwemo ya ubakaji , wizi, kutumia silaha na kuharibu mali.

Akiwasomea mashitaka yao Mkaguzi wa Polisi(PP) John Mwanzile makosa hayo yalifanyika Machi 11 hadi 15 mwaka huu, katika Kijiji cha Chilulumo wilayani humo kufuati vurugu za vyama vya siasa CCM na CHADEMA.

Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Yuda Paulo Siwiti (28), Agnasio Simchimba (37), Ivod Raphael Sichalwe (23), Danford Elias Simfukwe (22), Ally Simbeye (34), Happymax Simwaka (38) na Raymond Boniface (30).

Watuhumiwa hao wanakabiliwa na makosa hayo katika kesi namba 48, kupitia vifungu 296(i) a na b, 326(i) sura ya 16 marekebisho ya sheria mwaka 2012.

Mwendesha mashtaka hayo amesema pia watuhumiwa wametenda makosa katika vifungu vya 225, 297(a), 131(a)(i) na (ii), ambapo watuhumiwa wote walikana makosa hayo.

Aidha Yuda Paulo Siwiti, Happymax Simwaka na Raymond Boniface wote kwa pamoja wanakabiliwa na kosa la kubaka kwa kundi kinyume cha sheria cha kanuni ya adhabu, kifungu cha 131(a)(i) na (ii) cha mwaka 2002, watuhumiwa hao waliwabaka mabiti wawili wenye umri wa miaka 15 na mmoja mwenye umri wa miaka 20, bila ridhaa mnamo Machi 12 mwaka huu majira ya usiku wa saa 3:00 hadi saa 3:20.

Washtakiwa hao walikana kutenda kosa hilo na kunyimwa dhamana,  ambapo kesi hiyo itatanjwa tena April 3 mwaka huu.

Hata hivyo waliobakwa wameruhusiwa kutoka Hospitali ya Wilaya ya Mbozi na kurejea baada ya vipimo na matibabu, baada ya kulazwa katika hospitali hiyo Machi 18 kutokana na kupata matibabu hafifu katika Zahanati ya Chilulumo.

Wakati huohuo Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Chilulumo Adomali Leonard Nakambale (38), amefikishwa katika mahakama hiyo kwa makosa mawili yanayomkabili.

Mwendesha mashtaka Mazwile amesema tukio la kwanza ni kuvunja na kuiba mnamo Februari 29 mwaka huu, majira ya usiku.

Mwenyekiti huyo alivunja Ofisi ya Shule ya Msingi Chilulumo na kisha kuiba boksi moja la chaki, boksi la marker pen, vitabu viwili vya Atlasi, begi 20 chaki, Rim moja ya karatasi  vyote vikiwa na thamani ya shilingi 170,000/=.

Mwendesha mashtaka amesema kuwa kosa hilo ni kinyume cha sheria kifungu cha 96 a na b, sura ya 16 ya marekebisho ya sheria mwaka 2002 na mshtakiwa alikana kutenda kosa ambapo alidhaminiwa kwa dhamana ya maandishi ya shilingi laki 5.

Shtaka la pili linalomkabili Mwenyekiti huyo ni kutokana na kutoroka chini ya ulinzi halali wa Afisa mtendaji wa Kijiji saa 2 kamili asubuhi Februari 29 mwaka huu, Kijiji hicho usiku, kosa hilo lipo chini ya kifungu cha 116 na 125 sura ya 15 ya mwaka 2002.

Mtuhumiwa alikana kosa lake na kudhamini wa kwa shilingi laki mbili hadi April 10 mwaka huu, hadi kesi hiyo itakapotajwa tena.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger