Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mbeya imekataa ombi lililotolewa na mwekezaji wa Shamba la Kapunga Rice Project la kupewa pasipoti zao ili waweze kupata matibabu nje ya nchi.
Waliwasilisha ombi hilo mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Seif Kulita, mawakili wa watuhumiwa hao Ladslausi Rwekaza, Alei Rwechengula na Thomasi Mzerere wamesema watuhumiwa wote watatu wanakabiliwa na matatizo mbalimbali ya kiafya na wanatakiwa kusafiri kwenda nje ya nchi kimatibabu.
Kwa upande wake mwanasheria wa Serikali Grifini Mwakapeje ameiomba mahakama hiyo kutokubali ombi la washtakiwa kutokana na washtakiwa hao kuwa Raia wakigeni ambao ni Adries Daffe ambaye ni rubani, pia amedai kuwa leseni yake imekwisha, Walder Vermaak ambaye ni Meneja na Serger Bekker ambaye yeye ni Afisa Ugani na kwamba endapo watapatiwa pasipoti zao itakuwa rahisi kwa wao kukimbilia nchini kwao
Aidha amesema uchunguzi wa kesi hiyo bado haujakamilika kwa kukusanya vithibitisho kutoka kwa wananchi waliodhurika na tukio hilo.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi machi 28 mwaka huu itakapoanza kusikilizwa.
0 comments:
Post a Comment