Pages


Home » » KITUKO:- ALISHWA KINYESI MBELE YA MKEWE.

KITUKO:- ALISHWA KINYESI MBELE YA MKEWE.

Kamanga na Matukio | 05:03 | 0 comments

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Watu wawili wakazi wa Kijiji cha Isansu, Kata ya Vwawa, Wilaya ya Mbozi, Mkoani Mbeya wanakabiliwa na shtaka la shambulio la kudhuru kwa kumlisha vinyesi vyao mkazi mmoja wa mtaa hao mbele ya mkewe.

Washtakiwa hao ni pamoja na Joseph Kalinga na Ephrem Chisunga wakazi wa kijiji hicho na kosa hilo walimtendea Bwana Musa Kilalawima (42).

Mwendesha mashtaka wa Polisi PC Lugano Alfred Mwampulule amesema watuhumiwa walitenda kosa hili majira ya saa nane mchana kwenye bustani ya mlalamikaji.

Mlalamikaji wa kesi hiyo iliyovuta hisia za watu wengi wilayani humo Bwana ilisomwa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Vwawa Martha Malimi, ambapo mlalamikaji Bwana Musa aliiambia mahakama kuwa mnamo Machi 10 mwaka huu akiwa shambani na mkewe, watuhumiwa Joseph Kalinga na Ephrem Chisunga walimkamata na kisha kujisaidia vinyesi vyao.

Watuhumiwa wakiwa wameshika mapanga walimchukua mlalamikaji na kumpeleka mtoni na kumtaka asali sala ya mwisho kabla ya kuuawa huku mkewe akilia kwa uchungu, ndipo wakaanza kumlisha vinyesi hivyo kila mmoja kwa wakati wake na vingine wakimsiliba kichwani na sehemu mbalimbali, huku mikono yake ikiwa imefungwa kwa chuma na kamba.

Huku wakiendelea na ukatili huo mkewe wa mlalamikaji alifanikiwa kuwatoroka na kuendelea kupiga kelele, ndipo walimchukua Mussa hadi kijijini na kumtembeza mtaani hapo huku mwili mzima ukiwa umetapakaa kinyesi.

Mlalamikaji huyo amedai mahakamani hapo kuwa baada ya kuachiwa na watesaji haoa alitoa taarifa kwa Mjumbe wa mtaa aitwaye Julius Nyingi, ambaye naye alimtaarifa Mwenyekiti wa mtaa huo Rais Mwampashi, ambaye alitoa taarifa katika Kituo cha Polisi Vwawa na kufanikiwa kumkamata Joseph ambapo Ephrem alifanikiwa kutoroka.

Kwa upande wake mwendesha mashtaka PC Mwampulule amesema kosa hilo ni kosa la jinai kifungu cha 21 sura ya 16, cha kanuni ya adhabu cha mwaka 2002.

Hata hivyo mahakama hiyo ilikataa ombi la dhamana kwa mshtakiwa ambapo imedaiwa kuwa mtuhumiwa ana makosa mengine ya kujibu.

Kesi hiyo imeahirishwa mpaka April 10 mwaka huu, mlalamikaji atakapo leta mashahidi wake huku sheria ikiangalia ni kifungu gani sahihi cha sheria ya mtu kulishwa kinyesi, ambapo jalada la kesi hiyo limepelekwa kwa mwanasheria wa serikali ili ajaribu kuchambua.

Wakati huohuo watoto wawili John Mtawa (16) na Daniel Mwandingo (14), wamefikishwa mahakamani hapo kwa kosa la kuvunja na kuiba bidhaa kibandani kwa Tizo Mwasonga majira ya saa 5:00 usiku,  na kuiba tray 10 za mayai na viazi mviringo vyote vinathamani ya shilingi 91,000.

Mwendesha mashtaka wa Polisi PC Mwampulule, ameiambia mahakama hiyo chini ya hakimu Halima Malimi kuwa kosa hilo ni kinyume cha sheria kifungu cha 256 cha kanuni ya adhabu.

Watuhumiwa walitenda kosa hilo Machi 24 mwaka huukatika mtaa wa Ilembo wilaya ya Mbozi, ambapo watuhumiwa hao wamekana kutenda kosa hilo na kesi hiyo imeahirishwa mpaka April 11 mwaka huu na watuhumiwa wamepewa dhamana.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger