Pages


Home » » MWENYEKITI WA KIJIJI AUZA MABOMBA YA MAJI KAMA VYUMA CHAKAVU

MWENYEKITI WA KIJIJI AUZA MABOMBA YA MAJI KAMA VYUMA CHAKAVU

Kamanga na Matukio | 04:51 | 0 comments

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ileya, Kata ya Ifwekenya, wilaya ya Chunya mkoani Mbeya Bwana Stephen Joachim anatuhumiwa kuuza mabomba ya maji yaliyotandazwa na Mamlaka ya maji ya wilaya hiyo.

Mtuhumiwa anadaiwa kuuza mabomba hayo yaliyotandazwa eneo la Mbuyuni kama vyuma chakavu kwa mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mwaigaga mkazi wa Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini.

Bwana Stephen amefikishwa katika Mahakama ya wilaya hiyo, akituhumiwa kuuza mabomba hayo ambayo ni mali ya serikali, ambapo Mhandisi wa wilaya hiyo alitoa ushahidi mbele ya mahakama.

Kwa nia ya kujihami Mwenyekiti huyo amewafungulia mashitaka watu watatu, ambao walikuwa mstari wa mbele kutoa taarifa hizo akiwatuhumu wamemtukana na hivyo kufikishwa katika Mahakama ya mwanzo Mbuyuni .

Wananchi waliofunguliwa mashitaka hayo ni pamoja na Peter Mdula, Tatizo Sindilia na Jacob Mwanguku.

Hata hivyo wananchi wa Kijiji hicho wamemlalamikia Mwenyekiti huyo Stephen hatua aliyochukua kuwashtaki wananchi hao kwa kile kinachodaiwa kuwa anadhohofisha maendeleo katika Kijiji chao.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger