Pages


Home » » MTOTO ABAKWA NA ASKALI KISHA AFUNGIWA NDANI KWA MUDA WA SIKU TATU - MBEYA.

MTOTO ABAKWA NA ASKALI KISHA AFUNGIWA NDANI KWA MUDA WA SIKU TATU - MBEYA.

Kamanga na Matukio | 06:11 | 1comments
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Askali mmoja aliyefahamika kwa jina la utani Zungu ,mkazi yake mji mdogo wa Mbalizi jirani na Shule ya Sekondari Samaritan amembaka mtoto mwenye umri wa miaka 12, mwanafunzi wa darasa la sita wa Shule ya msingi Swaya Ntokela wilaya ya Rungwe.

Tukio hilo limetokea Machi 16 hadi 19 mwaka huu, ambapo mwanafunzi huyo amekatizwa masomo Machi 14, alipoenda kuchukuliwa na mama mmoja aliyefahamika kwa jina la Bi. Maida Ngulo ambaye ni mke wa askali huyo kwa nia ya kuwa mfanyakazi wa ndani.

Bi Maida alisafiri Machi 16 mwaka huu kuelekea Tukuyu na kumuacha mtoto huyo akiwa na Askali huyo(mumewe), ndipo usiku baada ya mtoto huyo kumaliza kumuandalia chakula askali huyo akitokea ulevini alimkamata binti(mtoto) huyo na kumbaka na kumjeruhi vibaya na kumfungia ndani kwa muda wa siku mbili, ambapo alijisahau kufunga mlango na mtoto huyo kutumia fursa ya kutoroka.

Lakini kutokana na ugeni mtoto huyo alikosa mahali kwa kwenda na kutokana na kitendo cha kubakwa alikuwa akishindwa kutembea na kuokotwa na msamalia mwema aitwaye Bi Lilian Costa na kumpeleka Kituo cha Polisi Mbalizi, ambapo alichukuliwa PF3 na kukimbizwa katika Hospitali Teule ya Ifisi kwa ajili ya kupima na mtoto huyo kugunduliwa amebakwa.

Aidha, Bi Lilian alirudisha taarifa Kituo cha Polisi  kuwa mtoto huyo kabakwa, ndipo juhudi za kumtafuta askali huyo kazini kwake kutokana na kitendo cha ukatili alioufanya hakuweza kufika kazini kwake na ametoweka nyumbani kwake pamoja na mkewe na simu ya mkewe imekua ikiita bila kupokelewa.

Hata hivyo mtandao huu unafuatilia kumrejesha mtoto huyo Shule ya Ntokela, ambapo pia inadaiwa jina lake limeuzwa kwa mtu mwingine na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, kutokana na mtoto huyo kutoonekana shuleni kwa muda baada ya mama yake kuumwa na ndipo walipotumia mwanya wa kumtorosha na kuja kufanya kazi za ndani.
Share this article :

1 comments:

crisocris ntokela said...

Ni hatua gani amechukuliwa Mwalimu huyo kwa kitendo alichofanya?

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger