Habari na Ezekiel Kamanga, Mbozi
Mabinti watatu waliobakwa katika vurugu zilizotokea hivi karibuni katika Kata ya Chilulumo wilaya ya Mbozi, mkoani Mbeya wamefikishwa katika Hospitali ya wilaya hiyo kwa ajili ya matibabu zaidi.
Mabinti wawili kati ya watatu wana umri wa miaka 15 kwa kila mmoja huku mmoja akiwa na umri wa miaka 20, mamefikishwa Machi 18 katika Hospitali hiyo baada ya kukutwa wamedhoofu kijijini baada ya kupatiwa huduma hafifu katika Zahanati ya Kijiji.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya hiyo Bwana Joseph Mwachembe baada ya kukuta mabinti hao wapo katika hali mbaya, kutokana na kulazimishwa kubakwa na kaka zao huku wakiwa wameshikiwa mashoka na kuvuliwa nguo zote.
Hata hivyo mabinti hao wakiongea kwa majozi makubwa walisema kuwa walibakwa na vijana waliowatambua kwa majina ya Shida Claud, Joseph Simfukwe, Marius Maswezi na wengine wengi ambao hawakuwatambua, ambapo tukio lilifanyika majira ya saa mbili usiku, Februari 12 mwaka huu.
Wakati huohuo viongozi wa Serikali ya kijiji wanadaiwa kulisimamia suala hilo la ubakaji, lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi yao.
CHADEMA imeweza kufungua jalada la madai dhidi ya watu waliohusika na tukio hilo kutokana na Bendera za chama hicho katika kata nzima zlishushwa na kuchomwa moto, ofisi kuvunjwa na baadhi ya mali kuchomwa moto.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama hicho kimetoa kauli mbiu isemayo "Wanachilulumo haki haiombwi kwa kupiga goti, bali kwa kupiganiwa" kwa hiyo wasikate tamaa.
Kauli hiyo imekuja siku chache mara baada ya kutokea kwa vurugu hizo zilizosababisha baadhi ya wananchi kuyakimbia makazi yao kwa hofu ya kuuawa.
0 comments:
Post a Comment