Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Watu watatu wamefariki mkoani Mbeya katika matukio matatu tofauti yaliyotokea mkoani hapa Februari mosi, mwaka huu.
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani hapa Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa matukio hayo na kusema majira ya saa 8:00 mchana katika kijiji cha Ikamasi wilaya ya Chunya mkoani hapa Japhary Khalfan Muyombe (31), mkuliwa na mkazi wa Kibaoni aliuawa baada ya kukatwakatwa kichwani kwa kutumia silaya ya jadi ya mapanga na watu wawili wasiofahamika ambapo amarehemu alikuwa akitokea shambani na kuelekea mtoni.
Chanzo cha tukio hilo ni tuhuma za wizi kwani marehemu alidaiwa kuiba kipimo cha dhahabu, ambapo mpaka sasa mmiliki wa kipimo hicho hajafahamika.
Tukio lingine limetokea majira ya saa 5 kamili asubuhi katika eneo la Forest ya zamani, ambapo mtu mmoja asiyefahamika jina wala makazi mwenye umri wa kuanzia miaka 25 hadi 30, jinsi ya kiume aliuawa na kisha kuchomwa moto.
Ambapo marehemu anadaiwa kuiba redio aina ya Subwoofer ambapo hakufahamika ni nani mmiliki wake na msakao mkali unaendelea ili kubaini watu waliohusika na tukio hilo.
Kamanda Nyombi amesema majira ya saa 6:30 mchana huko katika kijiji cha Haseketwa, wilaya ya Mbozi mtu mmoja aitwaye Bhangina Mukubwa (57), mkulima na mkazi wa kijiji cha hicho aliuawa na mtu mmoja aitwaye Funa Kamwela kwa kukatwa katwa na mapangashingoni kisha kuiba huku wawili, baiskeli aina ya Phonex na mbuzi wawili.
Chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi wa kugombea mashamba ya urithi na mtuhumiwa ametoroka mara baada ya upelelezi wa tukio hilo ukiendelea.
0 comments:
Post a Comment