Habari na Mwandishi wetu.
Mahakama ya mkoa wa Mbeya imewaachia huru Sadiki Mbango mkazi wa Air Port jijini Mbeya na Ibrahim Mponzi mkazi wa Chimala wilayani Mbarali ambao walikuwa wakituhumiwa na kosa wizi wa nyaya za umeme mali ya shirikala umeme nchini (TANESCO) zenye thamani shilingi milioni 16 laki saba ishirini na saba elfu mia tisa hamsini na nane.
Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Venasi Mlingi amesema mahakama inawaachia huru watuhumiwa hao baada ya ushahidi uliotolewa na TANESCO pamoja na shahidi aliyeandaliwa kutoa maelezo yanayotofautiana, jambo ambalo limeipelekea mahakama hiyo kuwaona watuhumiwa hao hawana hatia.
Aidha Katika mahakama ya mwanzo Mbalizi Richadi Mkwasa mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa Songwe viwandani amefikishwa katika mahakama hiyo kwa kosa la wizi.
Hakimu wa mahakama hiyo Jonasi Mwakyusa amesema mshatikiwa anatuhumiwa na kesi ya wizi wa kuvunja kisha kuiba mali zenye thamani ya shilingi milioni moja mali ya Frola Mwakyusa.
Mshtakiwa amekana shitaka linalomkabiliri na amerudishwa rumande kwa kukosa dhamana ya shilingi laki tano na kwamba kesi hiyo itasomwa tena machi mosi mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment