Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi.
*****
Habari na Mwandishi wetu.
Watu watano wamefariki dunia katika matukio tofauti mkoani Mbeya likiwemo la watu wanne kufariki dunia kutokana na ajali za barabarani.
Kaimu kamanda wa polisi mkoani Mbeya Barakiel Masaki amesema ajali ya kwanza imetoka eneo la Mwahala wilaya ya Mbeya vijijini ambapo gari aina ya Toyota Hiace yenye namba za usajili T.233 iliacha njia kisha kupinduka na kusababisha vifo vya watu wawili.
Tukio lingine limetokea kijiji cha Mabada Wilaya ya Mbarali ambapo pikipiki yenye namba za usajili T.304 BEB aina ya SUNLG ilimgonga mtoto Michael Mgaya mwenye umri wa miaka minne mkazi wa Lujewa na kusababisha kifo chake papohapo.
Aidha Masaki amesema Hakika Mwashilomba mwenye umri wa miaka 25 amefariki dunia baada ya pikipiki aliyokuwa anaendesha yenye namba za usajili T.550 AQV aina ya T.BETTER kugonga nyumba ambapo uchunguzi unaonyesha vyanzo vya ajali hizo ni mwendo kasi
Wakati huohuo kamanda Msaki amesema Teleza Mwankenja mwenye umri wa miaka 28 mkazi wa Ikombe wilayani Kyela ameuawa kwa kupigwa kwa kutumia kitu kizito na mumewake Fransisi Mwakyombe mwenye umri wa miaka 32 kutokana na ugomvi wa kifamilia.
0 comments:
Post a Comment