Vibanda vya biashara vikiwa vimefungwa katika Soko la Soweto jijini Mbeya.
*******
Habari na Mwandishi wetu
Wafanyabiashara wa soko la Soweto Jijini Mbeya wameiomba Serikali kukutana na wafanyabiashara kusikiliza kero zinazowakabili badala ya kutumia taarifa zinazotolewa na viongozi wa masoko ambao wamekuwa wakipotosha maamuzi yanayoafikiwa na wafanyabiashara.
Ombi hilo limetolewa na baadhi ya wafanyabishara wa soko hilo kufuatia kuwepo kwa utata wa ulipaji wa Ushuru na gharama za huduma ya choo.
Akitolea ufafanuzi wa kero zinazowakabili wafanyabiashara hao Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya Atanasi Kapunga amesema baraza limeadhimia mfanyabiashara kulipa ushuru wa shilingi mia mbili hadi shilingi mia tano.
Wakati huohuo amesema uongozi wa halmashauri utakwenda kuyafanyia kazi malalamiko yanatolewa na wafanyabiashara hao kuhusu kuzalilishwa na msimamizi wa choo.
Hata hivyo licha ya Meya wa jiji la Mbeya kuwaahidi wafanyabiashara hao kutekeleza madai yao, wafanyabiashara hao hawakuonesha kuridhishwa kutokana na kile walichokieleza kuwa wamechoshwa na ahadi zinazotolewa na viongozi mara kwa mara.
0 comments:
Post a Comment