Pages


Home » » MKAZI WA UYOLE APELEKWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUKUTWA NA KETE 26 ZA BANGI - MBEYA

MKAZI WA UYOLE APELEKWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUKUTWA NA KETE 26 ZA BANGI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 03:51 | 0 comments



Pichani ni Kete  za madawa ya kulevya.
*******
Habari na Mwandishi wetu.
Mapinduzi Magalasi mwenye umri wa miaka 34 mkazi wa Uyole jijini Mbeya amefikishwa katika mahakama ya mkoa kwa kosa la kukutwa na bangi kete ishirini na sita.

Akisoma shitaka hilo mbele ya hakim mkazi Francis Kishenyi mwanasheria wa serikali Achilesi Mlisa amesema Agosti 22 2011 maeneo ya Uyole mshitakiwa alikutwa na kete 26 za bangi kinyume na kifungu cha sheria namba 12 (d) sura 95 marekebisho ya mwaka 2002.

Hata hivyo mshitakiwa amekana shitaka hilo na amerudishwa rumande kwa kukosa mdhamini mwenye fedha shilingi laki mbili na barua kutoka kwa mtendaji na kesi hiyo itatajwa tena Februari 21 mwaka huu. 

Kwa hisani ya CHIMBUKO LETU
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger