Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Waganga wa jadi na tiba asilia mkoani Mbeya wamelitaka Jeshi la Polisi kutoa ushirikiano na watabibu wa asili ili kukomesha vitendo vya uovu vinavyohusishwa na imani za kishirikina.
Hayo yamebainishwa na watabibu wa tiba asilia na tiba mbadala katika mkutano ulio fanyikia katika ukumbi wa Shamba la Bibi uliopo katika eneo la Sokomatora Jijini Mbeya
Mwenyekiti wa mkutano huo Bwana Boniventura Mwalongo uliohusisha vyama vya ATME, MJATA ,CHAWATATA , na CHAUMUTA vinavyohusika na tiba asilia hizo amesema tiba zao zimekuwa zikihusishwa na imani za kishirikina kwa kuchochea vitendo vya upigaji nondo, mauaji ya maalbino(walemavu wa ngozi) na ubakaji ambapo asasi hizo hazija kanusha hadharani kutokana na baadhi ya watu kuvamia fani hiyo kwa nia ya kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.
Katika mkutano huo vyama hivyo vimeadhimia kupunguza vitendo vyote vya uovu vinavyofanywa na baadhi ya watu waliovamia fani hiyo kutoka nje ya nchi kwa kushirikiana na wa watanzania wasiosajiliwa wala kuwa na leseni ya kufanyia kazi hiyo.
Aidha wamelitaka Jeshi la Polisi kuwafichua hadharani wale wote wanaohusika na vitendo hivyo kwani wamekuwa wakifumbia macho licha ya kutajwa baadhi ya vigogo ambao ndio wenye mtandao huo.
Pia matabibu hao wa asili wamepiga vita marufuku matangazo yote ambayo hayana stahara katika vituo vya redio na matangazo yote yanayotoa matangazo yote yanayotangaza kuondolewa mara moja.
0 comments:
Post a Comment