Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi Blandina Nyoni
Mganga Mkuu wa Serikali Bw Deo Mtasiwa.(Picha na
Fununu Habari).
*********
Serikali imewasimamisha kazi katibu mkuu wa Wizara ya afya na ustawi wa jamii Brandina Nyoni na mganga mkuu wa Serikali Dokta Deo Mtasiwa ili kupisha uchunguzi wa vyombo vya dola juu ya tuhuma zinazowakabilia kuhusu mgomo wa madaktari unaoendelea hapa nchini.
Uamuzi huo umetolewa na waziri mkuu Mizengo Pinda wakati akizungumza na madaktari jijini Dar es salaam katika kutafuta suluhu ya mgomo.
Aidha amesema Mawaziri wanaodaiwa kuhusika na tuhuma za kusababisha mgomo huo watasubiri maamuzi ya Rais, pia amesema Serikali imeongeza posho ya madaktari wanaoitwa kwa ajili ya matibabu ya dharula kutoka shilingi elfu kumi hadi kufikia shilingi elfu ishirini na tano.
Kutokana na ongezeko hilo sasa Serikali itatumia zaidi ya shilingi bilioni 210 kabLa ya bajeti ya serikali ya mwaka 2012/2013
Hata hivyo Serikali imeunda kamati ya kushughulikia maadhimio nane yaliyowasirishwa katika mkutano huo.
0 comments:
Post a Comment