Habari na Mwandishi wetu.
Kati ya wanafunzi 605 waliochanguliwa kujiunga na elimu ya Sekondari kata ya Msangano wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya ni wanafunzi 120 ndio walioanza masomo yao huku wengine wakishindwa kuendelea na masomo kutokana na kutumikishwa kazi za shambani.
Hayo yamesemwa na mratibu wa elimu kata hiyo Bwana Osiah Mwanyemba wakati wa mahojino na mwandishi wetu ofini kwake kuhusu maendeleo ya elimu ya kata hiyo.
Bwana Mwanyemba amesema licha ya ufahulu mzuri wa watoto katika elimu ya msingi, wazazi wa wanafunzi hao wameonekana kuwa kikwazo katika maendeleo ya elimu kutokana na wazazi hao kuwatumikisha watoto wao mashambani.
Wakati huohuo amewataka wazazi kuwapeleka watoto wao shule walizochangulia na endapo mzazi atabainika kumnyima mtoto wake haki ya elimu atachukuliwa hatua za kisheria.
0 comments:
Post a Comment