Kabati lililohifadhiwa maandazi likiwa limewekwa kando kando ya maji machafu ambayo hutiririka kutoka chooni, kama inavyoonekana pichani. Ambapo mtando huu umeshuhudia tukio hili ndani ya Soko la Sokomatola jijini Mbeya.
Watoto hawa walikutwa wakicheza kando kando ya ghuba la kuhifadhia takataka lilolopo ndani ya soko la Sokomatola jijini Mbeya, hali ambayo inatishia kuambukizwa na magonjwa ya mlipuko ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa kipindupindu na kuhara.
Ghuba la kuhifadhia taka likiwa limefurika uchafu kutokana na Kitengo cha usafi wa mazingira kutoka Halmashauri ya jiji la Mbeya kutofika na kuuzoa uchafu huo kwa wakati muafaka. Hata hivyo ghuba hilo ni tegemezi kubwa la wafanyabiashara na wakazi wa mtaa katika kuhifadhi takataka katika Soko la Sokomatola
Mwenyekiti wa Soko la Sokomatola Bwana Shaibu Abdallah, amesema kutokana na ufinyu wa nafasi katika soko hilo wafanyabiashara wamekuwa wakilazimika kuhifadhi ndizi chini, licha ndizi hizo kuwekwa kandokando ya maji machafu ambayo hutiririka kutoka chooni.
Mwenyekiti wa Soko la Sokomatola Bwana Shaibu Abdallah, akionesha ghuba ambalo hutumiwa na wafanyabiashara na wakazi wa eneo hilo, ambapo amesema kwa takribani miaka saba mpaka sasa wamekuwa wakiiomba Halmashauri ya jiji kuwatafutia eneo jingine lenye nafasi kubwa, kutokana na eneo hilo kuwa finyu na wakati mwingine baadhi ya wakazi jirani hutumia ghuba hilo kutupa taka za majumbani na nyingine huwa na makaa ya moto hali inayotishia kuungua kwa soko hilo.
Pichani ni njia ambayo imekuwa ikitiririsha maji machafu kutoka chooni na ndizi zikiwa zimewekwa chini kandokando ya njia hiyo.
Ukuta wa choo cha Sokomatola ambao hutiririsha maji machafu, ambyo huwathiri wafanyabiashara na wateja wa soko hilo.(Picha na Ezekiel Kamanga, Mbeya).
0 comments:
Post a Comment