Pages


Home » » Mashabiki wa Mbeya City wafanya vurugu

Mashabiki wa Mbeya City wafanya vurugu

Kamanga na Matukio | 05:18 | 0 comments
.Mwamuzi Mbelwa anusurika kipigo

.Polisi walikuwa 4 washindwa kuwa kabili mashabiki

.Polisi Iringa wadaiwa kununua Mchezo mashabika washtukia

 Na Kenneth Ngelesi, Mbeya
MCHEZO wa ligi soka daraja la kwanza katika kundi B kati ya Mbeya City ya jijini na Polisi kutoka Iringa nusura uvunjike baada ya mwamuzi wa kati Simoni Mbelwa kutoka mkoani Pwani kunusurika kipigo kutoka kwa mashabiki wa M,beya City wakiamtuhunmu kuipendelea timu ya Polisi, mchezo huo ulipigwa katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine.

Hali hiyo ilitokea  wakati nmwamuzi huyo  akielekea kwenye vyumba vya kupumzikia ndipo kundi la mashabiki wa Mbeya City walimzingira na kuanza kumshambulia jambo lililo wapelekea Polisi kuingilia kati.

Hata hivyo hali ilikuwa mbaya zaidi kutokana na polisi kuwa wachache kwani walikuwa 4 uwanjani hivyo kuonekana kuzidiwa na mashabiki wa Mbeya City walikuwa na jazba hata hivyo hali ya utulivu iliejea.

Baadhi wa mashabiki walisikika wakitmtukana matusi ya nguoni mwamuzi huyo na kumlalamikia  kwa kitendo cha kuonyesha anaipendelea timu ya Polisi Iringa hata hivyo wakati huo tiku ya Polisi ilikuwa mbele kwa bao moja lilifungwa na mchezaji Juma Halifa namo dakika ya 45 ya mchezo.

‘Na nyie Polisi kama mnamsaidia mwamuzi kwa sababu anaipendelea  hiyo kwa kuwa ni timu ina milikiwa ja jeshi lenu tutakuwa hatu chezi na nyie kwa hiyo tutakuwa tukiwa gawia piont’walisikika washabiko, hata hivyo timu hiyo ya polisi haimikiwa ja jeshi hilo bali ilisha kabidhiwa kwa wananchi wa Iringa

Hata hivyo kitu kilicho pandisaha hasira kwa mashabiki wa Mbeya City kutaka kumpiga mwamuzi  Saimon  ni kutokana kutoa nje kwa kadi nyekundu mchezaji Moses Gogwin wa Mbeya City baada kumchapa kondea mchezaji wa Polisi Iringa.

Hata hivyo timu ya Mbeya City ilisazisaha bao kupitia kwa mchezaji Patrick Mwangungulu na hadio dakika 90 zinamalizika timu Meya City 1 na Polisi Iringa 1.

Mara baada ya mchezo huo kumalizika Tanzania Daima ilishuhudia katibu wa timu ya Polisi Abu Changali wakitolea maneno makali na mwenyekiti wa chama chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Mbeya Jonh Mwamwaja huku kili mmoja akituhumu kuwa kulikuwa na timu hizo kuhujumiana.

Katibu huyo wa timu ya Iringa Abu aliema kuwa kulikuwa na dalili zote za timu yake kuhujumiwa ndio maana washabiki waliamua kumvamia mwamuzi ili kuharibu ari ya mchezo, alisema kuwa watapeleka malalamiko yao ngazi inyo husika juu ya vurugu zilizo tokea.

 Naye mwenyekikti wa chama cha mpira wa miguu Mbeya MREFA John  Mwamwamaja aliesma kuwa timu ya Iringa ndio iliyo zoea kununua mechi kwa walivyo kuna kila dalili kushindwa ktika mchezo huo ndiyo wanasingizia vurugu za washabiki.

 Mwamwaja alitoa wito kwa shirikisho la mpira Tanzania TFF kuteua wamuzi wenye uwezo mkubwa na wasio na hata chembe ya tama ya pesa, kauli hiyo alitoa kutokana na minong’ono  ya chini kwa chini iliyo zagaa ksabkla ya mechi hiyo kuanza kuwa timu ya Polisi ilikuwa na mpango wa kununua mechi hiyo ili kujiwekea mazingira mazuri ya kuingia hatua ya tisa bora kutokana timu Mbeya City kuwa uhakika wa kusonga mbela kwani mpaka sasa imesha jikusanyia pointi  16 katibu wa Polisi Iringa  Abu alizikana tuhuma hizo.

Ligi hiyo ilitarajiwa kuendelea tena jana katika kundi B kati ya maafande wa magereza Tanzania Prisons waliwikaribisha  maafande wa jeshi la kujenga taifa  JKT Mlale kutoka Ruvuma mchezo uliotarajiwa kupigwa katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger