Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta Mohammed Gharib Bilal akisamilimiana na baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wakati wa ziara yake katika Mji mdogo wa Tunduma wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mheshimiwa Phillip Mulugo akijibu swali la Diwani wa Kata ya Tunduma Bwana Frenk Mwakajoka kuhusiana na zoezi la uandikishwaji wa watoto wa darasa ya la kwamba ambapo Waziri Mulugo amesema kuanzia siku ya Jumatatu Februari 26 watoto wote wanaostahili kwenda shule waanze masomo mara moja na ifikapo mwezi Aprili atakuja kukagua kama wanafunzi hao wamekwishaanza masomo..
Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta Mohammed Gharib Bilal akifungua lango la Soko la Tunduma lililoungua mwishoni mwa mwaka uliopita wakati wa ziara yake katika Mji mdogo wa Tunduma wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.
Baadhi ya halaiki ya wananchi wa Mji mdogo wa Tunduma wilaya ya Mbozi waliohudhuria katika ufunguzi wa Soko la Tunduma lililoungua mwishoni mwa mwaka uliopita.
Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta Mohammed Gharib Bilal akisamilimiana na mlemavu mwenye shati la blue Bwana Martine Teonas, wakati wa ziara yake katika Mji mdogo wa Tunduma wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.
Mkuu wa wilaya ya Mbozi Mheshimiwa Gabriel Kimoro wa kwanza kutoka kulia.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya mheshimiwa Abbas Kandoro akihutubia wananchi huku akiwasihi wananchi hao kumsikiliza Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta Mohammed Gharib Bilal wakati wa ziara yake katika Mji mdogo wa Tunduma wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.
Mkuu wa Kituo cha Polisi Tunduma A.S. Wendo (kulia) baada ya kutuliza mukali wa vijana wa Mji mdogo wa Tunduma, katika Ziara ya Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta Mohammed Gharib Bilal mjini hapo.
Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta Mohammed Gharib Bilal akiwahutubia wananchi wa Mji mdogo wa Tunduma wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya, wakati wa ziara yake ya uzinduzi wa vituo vya huduma za jamii, kama masoko n.k.
Mbunge wa Jimbo la Mbozi Magharibi Mheshimiwa David Silinde ambaye naye akiwaasa wananchi kuwa watulivu ili kumsikiliza Makamu wa Rais na kusahau yaliyotokea, ambaye anakuja kwa shughuli za Kiserikali na sio kisiasa na kama kuna tatizo lolote basi ni muda muafaka wa kumuuliza Makamu wa Rais ili kutafutiwa ufumbuzi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi, akipongezana na Diwani wa Kata ya Tunduma Frenk Mwakajoka baada ya kurejesha amani na utulivu wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta Bilal
Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mheshimiwa Phillip Mulugo (kulia), akipokea maelezo kutoka kwa Afisa Elimu mkoa Bwana Juma Kaponda (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Mbozi Mashariki mheshimiwa Godfrey Zambi (katikati) wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta Bilal
Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta Mohammed Gharib Bilal akisamilimiana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbozi, wakati wa ziara yake katika Mji mdogo wa Tunduma wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.
Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na wananchi wakati akiwasili katika Viwanja vya soko la Tunduma, wakati wa ziara yake katika Mji mdogo wa Tunduma wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.
Diwani wa Kata ya Tunduma Frenk Mwakajoka akitoa malalamiko kutokana na tatizo la kutofanyika kwa zoezi la uandikishwaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza.
Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Mwenyekiti wa Haki za Binadamu wilaya ya Mpya ya Momba Bwana Stephano Simwaza, wakati wa ziara yake katika Mji mdogo wa Tunduma wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.(Picha zote na Ezekiel Kamanga,Mbeya)
0 comments:
Post a Comment