Habari na Mwandishi wetu.
Madereva wa bajaji jijini Mbeya wamegoma kulipa Ushuru kutokana na kile walichokieleza kuwa hawawezi kulipa ushuru wakati miundombinu ya barabara wanayoitumia kuendelea kuwa mibovu.
Wakiongea huku wakionekana kuwa watu wenye jazba madereva hao wamesema kutokana na agizo la Serikali la kuwataka kutotumia barabara kuu hivyo nao hawakubaliani na suala la ulipaji wa ushuru.
Wakati huohuo madereva hao majira ya saa sita za mchana walikuwa wakionekana katika maeneo mbalimbali ya kata ya Iyela wakiwa katika harakati ya kuzitafuta bajaji mbili ambazo zinadaiwa kuwa zilikamatwa na watoza ushuru.
Kutokana na hali ya migomo ya mara kwa mara ambayo imekuwa ikifanywa na madereva wa bajaji, daladala na hata kwenye masoko Serikali haina budi kuangali upya utaratibu unaoutumia katika kukabiliana na kero za wananchi wa jiji la Mbeya.
0 comments:
Post a Comment