Habari na Mwandishi wetu.
Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Shamwengo Wilaya ya Mbeya vijijini Mkoani Mbeya aligongwa na moja ya mgari yaliyokuwa kwenye msafara wa Ziara ya siku tatu ya Makamu wa Rais Dakta Mohammed Gharib Bilal mkoani hapa.
Tukio hilo lilitokea majira ya saa kumi na mbili jioni Februari 25 mwaka huu wakati msafara wa magari wa kutokea Wilaya ya Mbarali kuelekea Jijini Mbeya.
Majeruhi alifahamika kwa jina la Franu Elia (28) ambapo aligongwa na gari hilo wakati akiendesha baiskeri wakati msafara huo ulipokuwa unapita.
Pia Franu aliokotwa na msamalia mwema Faines Mwalemba , Agnes Kahawa ambao waliomba msaada katika gari aina ya Hiace yenye namba za usajili T 247 BFL lililokuwa likiendeshwa na Bwana John Mgaya na msaidizi wake Justin Milaji ambao walimpeleka katika kituo cha polisi cha Inyala na kupewa PF3 na kisha kuelekea Kituo cha afya cha Inyala.
Hata hivyo kutokana na kujeruhiwa vibaya sehemu ya kichwani hali iliyopelekea kuvuja damu nyingi, wauguzi wa kituo cha afya Inyala walimtaka mgonjwa kupelekwe hospitali ya RUFAA jijini Mbeya, ambapo amelazwa mpaka sasa.
Lakini jitihada za kumtafuta Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa Advocate Nyombi ali aweze kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo ziligonga mwamba kutokana na Kamanda huyo kuwa katika msafara huo.
0 comments:
Post a Comment