Pages


Home » » TAARIFA ZA MAUAJI YA KUCHINJWA RAIA WASIO NA HATIA WILAYANI SONGEA-RUVUMA, FEBRUARI 2012.

TAARIFA ZA MAUAJI YA KUCHINJWA RAIA WASIO NA HATIA WILAYANI SONGEA-RUVUMA, FEBRUARI 2012.

Kamanga na Matukio | 01:57 | 0 comments

Wilayani Songea yapata watu wanne(4) wamechinjwa kikatili kwa siku tofauti tofauti na watu wasiofahamika na kwa sababu zisizojulikana fuatilia mtiririko wa matukio haya;-

· Mnamo tarehe kati ya 15 na 16.02.2012 mtu mmoja aliuawa kwa kuchinjwa na kisu katika maeneo ya Ruhwiko Wilayani Songea –Ruvuma.

· Tarehe 20.02.2012 siku ya Jumatatu alichinjwa mtu mwingine kutoka maeneo ya Rizaboni Wilayani Songea-Ruvuma kwa sababu zisizojulikana.

· Tarehe 21.02.2012 alichinjwa mtu mwingine.

· Tarehe 22.02.2012 kijana mmoja Dereva wa Boda Boda wilayani Songea alichinjwa kikatili nyakati za usiku akiwa nyumbani kwake baada ya kuitwa nje na mtu kwa madai ya kuwa kuna mtu anamazungumzo nawe.

Kimsingi matukio hayjo yote yamekuwa yakitokea nyakati za usiku,aidha Jeshi la Polisi Wilayani Songea limekuwa likifanya DORIA usiku pasipo mafanikio kwani matukio ya watu kuuawa bado yanaendelea kufanyika.

Hadi sasa ni watu WANNE(4) wameuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana na watu watano(5) wamejeruhiwa na Jeshi la Polisi leo asubuhi baada ya Jeshi la Polisi kutuliza GHASIA za wananchi wa Wilaya ya Songea wakifanya maandamano kuelekea katika Ofisa za Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa madai ya kuwa kwanini hawaoni jitihada za Serikali katika kudhibiti tatizo hilo,aidha majeruhi hao wamelazwa katika Hospital ya Mkoa

Nami nikiwa Mwanaharakati(Human Rights Deffender-THRD) Tunduru nitaendelea kuwajuza nini kinaendelea juu ya matukio haya.

Aidha naomba wanaharakati(THRDs) wote kufuatilia kwa karibu vyombo vya habari.
Chanzo cha taarifa;THRDs Wilayani Tunduru
Ndg.John Raphael Nginga
TUFAE EDUCATION AIDS TRUST
P.O.BOX 290,Tunduru
Fax;+255 25 2680001/81
Cell:+255 787 523030/765 636161/713 138525
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger