Pages


Home » » SHULE YA SEKONDARI YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA WANAFUNZI KUTOKANA NA IDADI YA VYUMBA VYA MADARASA- MBOZI

SHULE YA SEKONDARI YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA WANAFUNZI KUTOKANA NA IDADI YA VYUMBA VYA MADARASA- MBOZI

Kamanga na Matukio | 03:42 | 0 comments
Habari na Angelica Sullusi, Mbeya.
Shule ya Sekondari ya Kata ya Msangano Wilayani Mbozi inakabiliwa na upungufu wa wanafunzi kulingana na idadi ya vyumba vya madarasa vilivyopo shuleni hapo.

Akizungumza ofisini, Mratibu Elimu wa Kata hiyo  Osiah Mwanyamba amesema kuwa upungufu huo unatokana na ufaulu mdogo uliopo katani hapo kwa wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi.

Mwanyamba ametaja sababu inayofanya kuwepo na ufaulu mdogo katika shule za msingi katani hapo kuwa ni uhaba wa walimu katika shule hizo za msingi zipatazo tano,unaotokana na ugumu wa mazingira ya kufundishia kwa mwalimu lakini pia kujifunzia kwa mwanafunzi.

Ameongeza kuwa sababu nyingine ni uelewa mdogo wa wakazi wa maeneo hayo kwani bado wanakumbatia mila za zamani kwamba mtoto wa kike ni wa kuolewa tu,na hata wakiume hulazimika kwenda mashambani kulima hasa nyakati za msimu wa kilimo.

Aidha,Mwanyamba ameishauri serikali kutupia macho kata hiyo katika suala zima la kuboresha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia pamoja na kutoa elimu kwa wananchi wa maeneo hayo ili kuboresha elimu katani hapo.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger