Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mchungaji Elia Jongo wa kanisa la Church Of God la Air port jijini Mbeya baada ya eneo la alilokuwa ameazimwa kwa muda kwa ajili ya kuendeshea ibada na kudai kuwa eneo hilo kuwa ni lake.
Mchungaji Jongo alivamia eneo hilo linalomilikiwa na Bwana Allen Mwakyoma mwaka 2007 na kupiga hema ambalo alikuwa akiendeshea ibada bila kumwomba mmiliki wa eneo hilo ambalo aliliuza kwa Anyingisye Msokwa ambaye naye hakuwa ameliendeleza na hivyo mchungaji huyo kuendelea kufanyia ibada zake.
Sakata hilo liliingia sura mpya baada ya Februari 22 katika siku ya jumapili Anyingisye Msokwa kumwaga mawe katika eneo hilo na ambapo alimwambia mchungaji Jongo atafute eneo jingine lakini badala yake mchungaji alienda mahakamani Februari 23 na mahakama kuwataka Anita Mwakyoma na Anyingisye msouwa kupewa pingamizi na mahakama kutaka wasiliendeze eneo hilo.
Hata hivyo uchunguzi umebaini kuwa mchungaji hana nyaraka zozote zinazohusiana na eneo hilo licha ya kudai kuwa ni eneo lake na lina thamani ya sahilingi milioni arobaini kauli ambayo ilipingwa na bwana Allen Mwakyoma ambaye pia alipinga mkewe kuingizwa katika suala ambalo halimuhusu.
Hata hivyo Jeshi la polisi limelazimiaka kuingilia kati kwa kumtuma askari wake Pc Mbwana baada ya kupigiwa simu na mchungaji Jongo kwamba amevamiwa naye alipofika katika eneo hilo alikuta hali ndivyo sivyo na kudai hawezi kumkamata mtu yeyote bila kupata hati ya mahakama.
0 comments:
Post a Comment