.Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akiingia ndani ya ukumbi wa bunge leo mjini kuongoza kikao cha tisa cha mkutano wa sita wabunge ambapo bunge linahitimisha shughuli zake mjini Dodoma. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
*******
Habari na Chanzo Chetu.
Bunge limepitisha rasmi muswada wa sheria wa marekebisho ya sheria ya katiba mpya wa mwaka 2011 baada ya wabunge wote kuafikiana marekebisho yaliyomo katika muswada huo.
Awali kabla ya kupitishwa kwa muswada huo wabunge waliendelea na majadiliano ya muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya katiba ambapo kamati ya bunge ya katiba sheria na utawala imewasilisha bungeni marekebisho ya kifungu namba 17 cha marekebisho hayo ambapo jana Bunge ilishindwa kufikia makubaliano ya marekebisho hayo.
Baada ya taarifa hiyo wabunge waliiomba Serikali kutumia cheo kimoja kati ya mkuu wa wilaya na mkurugenzi wa halmashauri kuratibu shughuli za ukusanywaji wa maoni.
Kwa upande wake mwanasheria wa Serikali Fredrick Welema aliwataka wabunge kutii mamlaka iliyopo mbele yao kwa kufuata sheria.
Kwa niaba ya kambi rasmi ya Upinzani kiongozi wa kambi hiyo Free Man Mbowe aliwataka wabunge wanzake kufikia muafaka kwa maslahi ya Taifa.
0 comments:
Post a Comment