Pages


Home » » WANANCHI WAASWA KUTOJICHUKULIA SHERIA MKONONI, RAIA 11 WA NCHI YA ETHIOPIA WAKAMATWA.

WANANCHI WAASWA KUTOJICHUKULIA SHERIA MKONONI, RAIA 11 WA NCHI YA ETHIOPIA WAKAMATWA.

Kamanga na Matukio | 05:15 | 0 comments
Habari na Ezekial Kamanga, Mbeya.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi amewaasa wananchi kutojichukulia sheria mkononi kutokana na kauli mbiu hiyo kutopewa uzito na baadhi ya wananchi kukaidi na kuendelea kufanya mauaji kwa watuhumiwa wa wanaojihusisha na imani za ushirikina na wizi.

Tamko hilo limetolewa baada ya usiku wa kuamkia jana mtaa wa Meta, Kata ya Mbalizi Road wananchi wenye hasira kali kumuua mtu mmoja anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 25 hadi 30 kisha kumviringisha katika gurudumu la gari na kumchoma moto kwa tuhuma za wizi.

Hata hivyo wananchi hao walishindwa kubainisha mwananchi aliyeibiwa na mali iliyoibiwa na mtuhumiwa huyo katika mtaa huo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa huo Bi Halima Mwampyate amesema alisikia kelele na alipotoka nje alikuwa marehemu amekwisha uawa.

Kamanda  wa Polisi Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba jeshi lake linafanya uchunguzi ili kubaini waliohusika na tukio hilo na ameendelea kuwataka wananchi kutojichukulia sheria mkononi.

Aidha Nyombi amesema majira ya saa moja na nusu usiku eneo la Kasumulu wilayani Kyela, askari waliokuwa doria pamoja na idara ya uhamiaji, wamewakamata raia 11 wa nchi ya Ethiopia, ambao waliongozwa na Bwana Getachu Dine (35) raia wa nchi hiyo, ambao waliingia nchini bila kibali.

Mbali na hao Watanzania wawili Bwana Joackim Chinika (33) na Lazaro Mwaisaka (24), wamekamatwa baada ya kuwasindikiza raia hao kupitia njia za maficho.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger