Pages


Home » » BAADA YA UKIMYA WA MUDA MREFU:- SERIKALI YAMFIKISHA MAHAKAMANI MWEKEZAJI WA MASHAMBA YA KAPUNGA - MBEYA

BAADA YA UKIMYA WA MUDA MREFU:- SERIKALI YAMFIKISHA MAHAKAMANI MWEKEZAJI WA MASHAMBA YA KAPUNGA - MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:46 | 0 comments
 Rubani wa ndege Andries Daffe iliyotumiwa kunyunyizia sumu katika mashamba ya eneo la Mpunga mmoja ambazo ni hekati 489.5 za mazao ziliathiriwa na sumu hiyo,  akiwa na mkewe baada ya kudhaminiwa.
Jengo la Mahakama ya Kuu mkoa wa Mbeya
*****
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Mwekezaji wa Shamba la KAPUNGA lililopo Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya na Kampuni ya Export Trading Group amefikishwa mahakama ya wilaya ya Mbeya, kwa makosa mawili tofauti likiwemo la kula njama ya kutenda kosa la kuharibu mali na kuharibu mali za wananchi kwa hila.
Mwekezaji huyo alifikishwa mahakamani hapo jana, kwa makosa hayo aliyoyatenda Januari 12 na 14 mwaka huu kwa kutumia ndege ya kunyunyizia dawa ambapo alimwaga sumu katika mashamba ya wakulima zaidi ya 154 wa kijiji cha Kapunga wilayani humo.
Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo Seif Kulita, mwendesha mashtaka wa serikali Griffin Mwakapeje alisema kuwa washitakiwa ambao ni Meneja wa shamba hilo Walder Vermaak, Afisa Ugani Serger Bekker na Rubani wa ndege Andries Daffe walitenda kosa hilo wilayani humo na kuharibu mazao ya wakulima hekari 489.5.
Bwana Mwakapeje alisema wawekezaji hao kwa pamoja walitenda kosa ambalo ni kinyume cha sheria namba 226(i) cha marekebisho ya sheria ya mwaka 2002, la kuharibu mazao hayo ya mpunga wa wakulima eneo linalojulikana kwa jina la Mpunga mmoja.
Baada ya mashtaka hayo, Hakimu Kuliata alipowauliza washtakiwa wote kwa pamoja walikana shtaka hilo ambapo Wakili anaowatetea watuhumiwa hao Ladislaus Rwekaza aliomba dhamana kwa wateja wake na hatimaye mahakama ikaridhia kwa masharti ya kila mtuhumiwa kuwa na mdhamini mmoja mwenye mali isiyohamishika isiyopungua shilingi milioni 10.
Aidha Hakimu huyo alitoa sharti kwa watuhumiwa hao kuwa mbali na sharti la kuwa na mdhamini mmoja na mali isiyohamishika pia watuhumiwa alitakiwa kukabidhi hati ya kusafiria na kwamba hawapaswi kusafiri nje ya mkoa wa Mbeya na kama watahitaji kusafiri nje ya mkoa ni lazima wapate kibali cha mahakama hiyo ambapo washtakiwa walitimiza masharti hayo.
Baada ya masharti hayo watuhumiwa walidhaminiwa na Uwesu Msumi mkazi wa jiji la Dar es salaam na kukabidhi nyumba yenye namba 229 Block J iliyopo Mbezi jijini humo,  mwingine ni Bwana Christian Basil Mmas aliyekabidhi hati ya nyumba yenye namba 109 iliyoo Ulole Jijini humo na Bwana Sunnil aliyetoa hati ya nyumba yenye namba 254 iliyopo Kigamboni jijini humo na kesi hiyo itatajwa tena Machi 6, mwaka huu.
Baadhi ya wananchi walioathiriwa na sumu hiyo wakati ndege ikimwaga sumu mashambani na kushuhudia ni pamojana Bwana Michael Shija, Severina Mbwilo, Elikana Nsemwa, Edward Simkoko, Gaidon Peter Ngogo, Jailo Esao (20), Jackson Mwandemange (52), Catherina Shipela (50), Edda Ngosha (35) na Ramadhan Nyoni (50).
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger