Pages


Home » » MWENYEKITI WA MTAA AMTAPELI MFIWA SHILINGI 5,000/= AJIHAMI KWA KUWASHITAKI VIJANA WALIOCHIMBA KABURI - MBEYA

MWENYEKITI WA MTAA AMTAPELI MFIWA SHILINGI 5,000/= AJIHAMI KWA KUWASHITAKI VIJANA WALIOCHIMBA KABURI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:05 | 0 comments

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Kaimu mwenyekiti wa mtaa wa Ivwanga katika Kata ya Iwambi Jijini Mbeya amejikuta kuingia matatani baada ya kumtoza mfiwa jumla ya shilingi elfu tano kwa ajili  ya vijana wa mtaa huo wa Ivwanga kwa ajili ya kuchimbia kaburi.

Mwenyekiti huyo anayejulikana kwa jina la Nicholousi Njoua amedaiwa kujipatia shilingi elfu tano kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa mchungaji Amoni Mahava aliye fiwa na mwanaye Februari 4 na kuzikwa Februari 7 mwaka huu katika makaburi ya Iwambi jijini hapa.

Katika siku ya mazishi Njoua alimtaka mchungaji kulipa shilingi elfu tano kwa ajili ya vijana waliokuwa wakichimba kaburi kitu ambacho si kweli kwani mwenyekiti huyo alizichukua na kuziweka mfukoni mwake hali iliyopelekea  iliyopelekea kuwaudhi vijana wa mtaa huo mara kadhaa aliendelea kumbugudhi mfiwa akimtaka  atoe pesa hizo vinginevyo vijana wasingechimba kaburi.

Baada ya mchungaji Mahava kukerwa na kauli  za Njoua  aliamua kulipa pesa hizo na kuamua ndugu wawapelekee vijana wanaochimba kabuli na kufanya mgomo ndipo ndugu walikuta kaburi limemalizika mapema walishangazawa na kauli ya mwenyekiti  hivyo ndipo walipo mwamuru azirejeshe mara moja kutokana na amri ya mfiwa na akafanya hivyo.

Kutokana na hali hiyo Nichalous Njoua hakutokea tena katika  msibani badala yake Februari 8 aliamua kuwafungulia mashitaka katika baraza la kata ya Iwambi akidai kuwa baadhi ya vijana wameleta fujo makaburini ambao ni Ibu Gibsoni,Juma Mwanzalizya,Ezekieli  Anangisye ,Osward Mwaka Swala ,Zainabu Mjaliwa Omali Wanga Na Mama Doto ambao walifikishwa katika baraza la kata ya Iwambi Februari 10 na kusomewa shitaka hilo.

Katika hali ya  kushangaza Njoua na mtendaji wa mtaa Jacobu Sanga  hawakutokea barazani ndipo waliamriwa kufika Februari 14  mwaka huu walipofika siku  hiyo mwenyekiti Njoua hakufika badala yake  mtendaji alidai suala hilo limefutwa  hivyo vijana hao wapo huru jambo lililowaudhi vijana hao waliosindikizwa na wenzao 8 na kuomba kuandika barua ya hakimu au mwenendo wa shauri lao na baraza kukataa katakata ombi la vijana hao.

Alipoulizwa mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji  Juma Iddi amesema kuwa halmashuri yake haina utaratibu wa kumtoza mfiwa pesa kwa ajili ya kuchimba kaburi inao utaratibu wa kutoza katika makaburi ya sabasaba na maeneo mengine hayatozwi malipo yoyote

Pia mkurugenzi huyo ameongeza kuwa suala hilo atalifuatilia ili kujua mwenyekiti alipataje jukumu la kutoza pesa bila stakabadhi kama yalikuwa malipo halali  kwani pesa zote za halimashuri hutolewa stakabadhi.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger