Habari na Ezekiel Kamanga, Tunduma.
Vurugu zilizotokea katika mji wa Tunduma wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya kabla ya kuwasili Makamu wa raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Mohammed Gharib Bilali.
Vurugu hizo zilitokana na watu wasiofahamika kung’oa bendera za Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambapo ilimlazimu Diwani wa Kata ya Tunduma Frenk Mwakajoka na Mkuu wa kituo cha Polisi Tunduma Bwana A.S.Wendo kuwa na wakati mgumu kuwatuliza vijana hao waliokuwa na mukali kabla ya Makamu wa Raisi kuwasili eneo hilo kwa ajili ya kuzindua soko la Mji mdogo wa Tunduma lililoungua mwishoni mwa mwaka jana.
Aidha Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa Advocate Nyombi aliwasihi wananchi wa eneo hilo kuwa watulivu na kuwataka wakazi wa eneo hilo kuondoa bendera zao kwa ajili ya kuheshimu mamlaka kwani kiongozi huyo hana itikadi ya chama chochote na bali anawakilisha Serikali.
Kwamjibu wa wananchi wa eneo hilo walidai kuwa bendera zao za vyama pinzani kuwa zimeng’olewa bila ridhaa yao.
Hata hivyo sakata hilo lilitulizwa na Mbunge wa Jimbo la Mbozi Magharibi Mheshimiwa David Silinde ambaye naye aliwaasa wananchi kuwa watulivu ili kumsikiliza Makamu wa Rais na kusahau yaliyotokea, ambaye anakuja kwa shughuli za Kiserikali na sio kisiasa na kama kuna tatizo lolote basi ni muda muafaka wa kumuuliza Makamu wa Rais ili kutafutiwa ufumbuzi.
Wakati huo huo Silinde ameongeza kuwa ameweza kufanya mazungumzo na mweshimiwa Dokta Slaa kuhusiana na kutokea kwa tukio hili hivyo naye amewaomba wananchi wamsikilize Makamu wa Rais ikiwa ni kutoa matatizo yanayowasumbua bila kufanya vurugu zozote.
Mheshimiwa Makamu wa Rais Dakta Mohamed Gharib Bilali kabla ya yote aliwashukuru wananchi wa Tunduma kwa ujenzi wa soko hilo ikiwa ni kutoa pole kwa watu wote walioathirika na janga la moto lililotokea hivi karibuni na kuharibu mali za watu na kwamba Seriakali inaangalia ni namna gani inaweza kuwasaidia waathirika hao.
Aidha Bilali aliahidi kutoa ushirikiano wa dhati ili kuwa nusuru wale wote walioathirika na janga hilo na kuwataka wananchi wa eneo hilo kuwa na hulka ya kuwamini vingozi wao kwakile wanachokizungumza.
Baada ya kuhutubia wananchi hao Makamu wa Raisi alimkaribisha Mbunge Silinde ili kupokea kero zinazowasibu wananchi jimbo lake, ambapo Mbunge huyo amesema kuwa amesisitishwa na maamuzi ya Serikali kusitishwa uandikishwaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza kwa mwaka huu, ambapo alimtaka Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bwana Philip Mulugo kujibu swali hilo.
Kwa upande wake Waziri Mulugo amesema kuanzia siku ya Jumatatu Februari 26 watoto wote wanaostahili kwenda shule waanze masomo mara moja na ifikapo mwezi Aprili atakuja kukagua kama wanafunzi hao wamekwishaanza masomo..
Kwa mjibu wa mheshimiwa diwani Frenk Mwakajoka amesema kuwa tangu Mwaka 2005 wanaupungufu wa vyumba vya madarasa 214, hivyo amemuomba Makamu wa Rais kumuonya Afisa Elimu wa mkoa wa Mbeya Bwana Juma Kaponda kutoendelea kutoa maamuzi ambayo yanawaathiri na kudidimiza elimu mkoani hapa na awe tayari kupokea ushauri ili kuondoa ujinga.
0 comments:
Post a Comment