Pages


Home » » Wakazi wa kijiji cha Kapunga wilayani Mbarali mkoani Mbeya wameingia hasara ya shilingi milioni 718

Wakazi wa kijiji cha Kapunga wilayani Mbarali mkoani Mbeya wameingia hasara ya shilingi milioni 718

Kamanga na Matukio | 06:00 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbarali
Wakazi wa kijiji cha Kapunga wilayani Mbarali mkoani Mbeya wameingia hasara ya shilingi milioni 718 kutokana na mwekezaji wa mashamba ya Kapunga rice project kumwaga sumu ya kuua mimea, kwa kutumia ndege.

Mwekezaji huyo alifanya tukio hilo Januari 12 hadi 14, mwekezaji kwa kutumia ndege ya kunyunyizia dawa alimwaga sumu hiyo katika mashamba yake, pia na katika mashamba ya wananchi katika eneo linalofahamika kwa jina la Mpunga mmoja, na kusababisha wakulima zaidi ya 154, wanaomiliki zaidi ya hekari 4600 na heka 5.

Meneja Mkuu wa shirika la Kapunga Rice Project Wally Vermaak amesema ataendelea kufanya hivyo hadi hapo wananchi hao watakapo acha kutumia ardhi anayoimiriki.

Hadi sasa ni wananchi Baadhi ya wananchi 8 akiwemo afisa mtendaji wa kijiji hicho Raphael Moreli mwenye umri wa miaka 44 wameshaathirika na sumu hiyo.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mbarali Luteni Kosimasi Kayombo amesema tume aliyoiunda kuchunguza tukio hilo bado inaendelea na uchunguzi.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger