Pages


Home » » DC MBEYA :- SERIKALI IMESHTUSHWA NA TUKIO LA MVUA KUBWA ZA MAWE ZILIZONYESHA KATIKA KIJIJI CHA NSAMBYA SONGWE.

DC MBEYA :- SERIKALI IMESHTUSHWA NA TUKIO LA MVUA KUBWA ZA MAWE ZILIZONYESHA KATIKA KIJIJI CHA NSAMBYA SONGWE.

Kamanga na Matukio | 03:52 | 0 comments
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Bwana Evans Balama(kushoto) akiwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbeya maarufu kama Ndomboro, katika moja ya vikao vya kujadili masuala mbalimbali ya kutatua kero za wakulima .(Picha na Maktaba yetu)
******
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Evans Balama, amesema kuwa serikali imeshtushwa na tukio la mvua kubwa za mawe zilizonyesha katika kijiji cha Nsambya Songwe na kuharibu hekari 248 za chakula na kuziacha familia 68 zikiwa hazina kitu.

Balama amesema alipokuwa akipokea msaada wa mifuko 100 ya saruji iliyotolewa na kampuni ya Tunakopesha Limited tawi la Mbeya kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa mtaa wa Ikuti, kata ya Iyunga waliokumbwa na mafuriko makubwa Desemba mwaka jana.

Akipokea msaada huo toka kwa meneja wa tawi hilo, Job Mwakyoma, kwa ajili ya waathirika wawaliobomokewa nyumba 22, vyoo 30 na nyumba nyingine 40 kuharibika, Balama amesema msaada huo utawawezesha baadhi ya wananchi kuweza kujenga upya makazi yao.

Alieleza madhara ya mvua hiyo iliyonyesha kwa muda wa saa 18 kwa wakazi wa kijiji cha Nsambya kuwa ziliharibu hekari 248 za mazao zikiwa ni 122 za mahindi, 96 za maharage, 17 nukta 5 za kahawa na 10 nukta 5 za migomba.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger