Wazee wa kimila mkoani Mbeya kwa kushirikiana na Kikundi cha Polisi jamii ulinzi shirikishi wamendelea kupinga na kukemea vitendo vya upigaji nondo, mauji ya watoto wasio kuwa na hatia na wizi wa mali za watu unaofanywa na baadhi ya watu.
Hayo yalisemwa na mwenyekiti wa chama cha MJATA mkoani hapa Bwana Shayo Soja Makoko alipokuwa akihutubia katika mkutano uliofanyikia katika kijiji cha Nsanga Mwelu Mbeya vijijini ambapo mkutano huo ulihudhuriwa na machifu kutoka wilaya mbalimbali zilizopo mkoni hapa wakishirikiana na kikundi cha polisi jamii.
Chifu Makoko alisema kuwa chama hicho kipo kwa ajili ya kupambana na maovu yote yanayojitokeza katika ndani ya jamii ili kuhakikisha matatizo yanayojitokeza katika jamii zetu kuhakikisha yanaondolewa mara moja.
Aidha Makoko aliongeza kuwa chama cha MJATA kilianzishwa na mchifu kwa lengo la kusaidiana na serikali kwa lengo la kupambana na kukomesha vitendo vya kiovu ndani ya jamii.
Naye mjumbe kutoka katika kikundi cha polisi jamii mkoani hapa Bwana Pita Mwakasembwa aliwataka wananchi pamoja na machifu kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi badala yake washirikiane na Jeshi la polisi katika kutoa taarifa zinazojitokeza katika jamii pindi wahalifu wanapowakamata.(Kwa habari zaidi soma hapa Chimbuko Letu Blog)
0 comments:
Post a Comment