Habari na Mwanishi wetu
Watu wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti mkoani Mbeya yaliyotokea Februari 26 mwaka huu.
Katika tukio la kwanza lilitokea majira ya saa nane mchana katika eneo la Nzovwe katika barabara ya Mbeya/Tunduma ambapo Hamisi Fusa (35), mkazi wa Simike aligongwa na gari lisilofahamika .
Chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa jijini Mbeya na huku Jeshi la polisi likifanya uchunguzi juu ya tukio hilo.
Na katika tukio jingine ambalo lilitokea Tunduma katika wilaya ya Mbozi mkoani hapa mtu mmoja asiyefahamika jina lake (20) aliuwawa na watu wasiofahamika baada ya kukatwa katwa na vifaa vyenye ncha kali kisha mwili wake kutupwa katika moja ya madarasa ya shule ya msingi Tunduma.
Na chanzo cha mauaji bado hakijafahamika na Polisi bado wanafanya uchunguzi juu ya tukio hilo.
Adha katika majira ya saa tano asubuhi mwendesha pikipiki asiyefahamika katika eneo la Chimala katika barabara ya MBEA/IRINGA aliingilia kati msafara wa Makamu wa Rais alipokuwa anaelekea mkoani Iringa na kusababisha moja ya magari kupinduka .
Gari lenye namba za usajili STU 2429, ambapo ndani ya gari hilo lililopinduka alikuwemo Mbunge wa Viti maalum wa mkoa wa Mbeya (CCM) Hilda Ngoye, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Beatha Swai pamoja na dereva wa gari hilo wamekimbizwa katika hosipitali ya Rufaa mkoani Mbeya.
0 comments:
Post a Comment