Mmoja wa majeruhi wa kati ya 40 walionusurika kifo baada ya basi
waliokuwa wakisafiri aina ya Coaster, lenye nambari za usajili T 374 AVR,
kupinduka lilipogongwa kwa nyuma na basi jingine la kampuni ya El Saedy lenye
nambari T 499 AVG. Tukio lililotokea Aprili 23 mwaka huu saa moja asubuhi eneo la Imezu na Inyala Wilaya ya Mbeya Vijijini.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya
Sekondari Imezu wakikwa katika Hospitali ya Rufaa, wakisubiri kupatiwa
matibabu, mara baada ya basi aina ya Coaster waliyokuwa wakisafirikia enye nambari za usajili T 374 AVR,
kupinduka lilipogongwa kwa nyuma na basi jingine la kampuni ya El Saedy lenye
nambari T 499 AVG. Tukio lililotokea Aprili 23 mwaka huu saa moja asubuhi eneo la Imezu na Inyala Wilaya ya Mbeya Vijijini.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Imezu wakikwa katika
Hospitali ya Rufaa, wakisubiri kupatiwa matibabu, mara baada ya basi
aina ya Coaster waliyokuwa wakisafirikia enye nambari za usajili T 374 AVR,
kupinduka lilipogongwa kwa nyuma na basi jingine la kampuni ya El Saedy lenye
nambari T 499 AVG. Tukio lililotokea Aprili 23 mwaka huu saa moja asubuhi eneo la Imezu na Inyala Wilaya ya Mbeya Vijijini.
Basi aina ya Coaster waliokuwa wakisafiria abiria zaidi ya 40, lenye nambari za usajili T 374 AVR,
likiwa limepinduka baada ya kugongwa kwa nyuma na basi jingine la kampuni ya El Saedy lenye

nambari T 499 AVG.
Basi la kampuni ya El Saedy lenye
nambari T 499 AVG lililohusika katika ajali, baada ya kuligonga kwa nyuma basi aina ya Coaster enye nambari za usajili T 374 AVR ambapo zaidi ya abiria 40 kunusurika kifo.
Tukio lililotokea Aprili 23 mwaka huu saa moja asubuhi eneo la Imezu na
Inyala Wilaya ya Mbeya Vijijini.(Picha na Ezekiel Kamanga, Mbeya.)
*******
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Abiria
zaidi ya 40 wamenusurika kifo baada ya basi waliokuwa wakisafiri aina ya
Coaster, lenye nambari za usajili T 374 AVR, kupinduka lilipogongwa kwa nyuma na
basi jingine la kampuni ya El Saedy lenye nambari T 499 AVG.
Kwa mujibu
wa mashuhuda wa basi la El Saedy likiwa katika hali ya mwendokasi liliharibika
mfumo wa breki kutoka eneo la Mlima Nyoka na kuligonga basi hilo dogo kwa nyuma
katika mteremko wa Shule ya Sekondari Imezu, hali iliyopelekea basi hilo dogo
kupinduka.
Baada ya
Coaster kupinduka basi la El Saedy likiwa bado katika mwendokasi liliendelea na
safari, kabla ya dereva kufanikiwa kulichepusha kabla halijavuka reli ya TAZARA
katika Kijiji cha Inyala Wilaya ya Mbeya Vijijini.
Aidha baadhi
ya abiria katika basi hilo dogo walikuwemo wanafunzi 28, wa kike na kiume
wakielekea shuleni majira ya saa moja asubuhi, Aprili 23 mwaka huu katika Shule
ya Sekondari Imezu.
Mara baada
ya ajali hiyo kutokea baadhi ya abiria walikuwemo katika basi hilo dogo
walikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa Jijini Mbeya, ambapo kati yao wamelazwa
ili kufanyiwa uchunguzi na wengine wakiruhusiwa kurudi nyumbani.
Kaimu
Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Mbeya Barakiel Masaki,hakupatikana
kuelezea ajali hiyo ingawa dereva wa basi la El Saedy anashikiliwa na Polisi
kwa mahojiano.
Wakati huo
huo watroto watano waliokuwa wakioga katika mfereji wa Mwanjejele, uliopo
Igurusi Wilaya ya Mbarali, Aprili 22 mwaka huu majira ya saa tisa
alasiriwaliokota begi lililokuwa linaelea katika maji ya mfereji huo na kukuta
maiti ya mtoto mchanga.
Maiti hiyo
ikiwa imeharibika vibaya kutokana na kuoza ndipo walipolichukua begi hilo na
kulikabidhi katika Kituo cha Polisi cha Igurusi.
Hata hivyo
hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusika na tukio hilo, licha ya wimbi la kuuawa
kwa watoto wachanga Mkoani Mbeya limekuwa tatizo hali inayosababisha vifo kwa
watoto wasio na hatia.
0 comments:
Post a Comment