Mfugaji
Bwana Mungo Makubi (27) kushoto na Singu Mwakami (23) wakimtazama
ng'ombe aliyeuawa kwa kugongwa na gari aina ya Toyota Landcruiser lenye
nambari ya usajili T 566 BQH. iliyokuwa ikiendeshwa na mwekezaji wa
Kapunga Rice Project wilayani Mbarali aitwaye Bwana Gerry Baquzein baada
ya kuwakosa wafugaji hao baada ya kujistiri nyuma ya mti na kisha
hasira za mwekezaji kuishia kwa kumgonga ng'ombe huyo mwenye thamani ya
shilingi laki 6 za kitanzania na kisha kufa papo hapo. (Picha na Maktaba yetu).
*******
Habari Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Tume iliyoteuliwa na Mkuu wa Mkoa wa
Mbeya Mheshimiwa Abbas Kandoro, imeanza kazi ya kupima eneo la mipaka
ili kujua uhalali wa pande hizo mbili zinazopingana kwa muda wa miaka
sita sasa, ambapo kijiji hicho kimeshindwa kufanya shuguli za
kimaendeleo kutokana na mwekezaji huyo (Kapunga Rice Project)
kuwanyanyasa wananchi hao.
Wakati tume hiyo ikiwa imeaanza kazi
rasmi Aprili 19 mwaka huu, imeshuhudia mwekezaji huyo akibandika
matangazo ya kuwataka wananchi wasipite maeneo kadhaa na kwamba
atakamata mifugo, baiskeli, pikipiki, magari na waenda kwa miguu na
kuwatoza faini watakapokiuka agizo hilo.
Amesema faini hizo zinaanzi shilingi
20,000 hadi 100,000 hali ambayo imepingwa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho
Bwana Ramadhan Nyoni pamoja na Halmashauri ya kijiji hicho na kuitaka
tume hiyo ione yenyewe ukatili unaofanywa na mwekezaji huyo.
Aidha ni takribani miaka 6 mwekezaji
huyo hajaweza kuendeleza kijiji hicho na kuhodhi shule, zahanati, miundo
mbinu ya maji na umeme na hivyo kijiji hicho kuwa kama kisiwa na
kuwafanya wananchi hao kuishi kama watumwa katika ardhi yao.
Baadhi ya wajumbe walioteuliwa katika
Tume hiyo ya uchunguzi ni pamoja na Mwenyekiti Bi Frola Luvanda
(Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda), Sospeter Kajuna (Afisa mipango
Mkoa), Geofrey Mwaijobele (Afisa Mipango Wilaya ya Mbarali), Omary
Mataka (Mpima Ardhi) na Enock Kyando (Afisa Mipango Mkoa).
Wengine ni Saimon Mlimandago na
Clemence Mero ambapo tume hiyo itafanya kazi mpaka May 14 mwaka huu
katika upimaji wa awali imeoneshwa na wananchi mipaka asili kabla ya
kijiji hicho kulikabidhi Shirika na NAFCO ambalo lilipewa ardhi hiyo
bure kwa ombi rasmi la Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere, 1989 na kuanza rasmi mradi wa umwagiliaji 1993.
Hata hivyo uongozi wa Kijiji umeitaka
tume hiyo kutenda haki ili kwani eneo waliloikabidhi NAFCO kipindi
hicho ni hekari 5,500 badala ya 7,370 zinazodaiwa hivi sasa na mwekezaji
kuwa ndizo alizouziwa ambapo hakunaukweli wowote na kijiji hicho
kuonekana kipo ndani ya eneo la mwekezaji.
Wakati
huo huo baadhi ya kare wanazozipata ni pamoja na kukamatwa mifugo na
kuuawa, kuzuia kupitisha mazao kijijini hapo na mwekezaji huyo kushindwa
kuyaendeleza mashamba hayo na kuwakodisha wananchi, kwa hiyo serikali
iangalie upya kwani mwekezaji huyo hainufaishi Kijiji wala taifa.
0 comments:
Post a Comment