Meneja wa benki hiyo wa wilaya ya Mbozi, Mkoani Mbeya Bwana Cornelius Msigwa, akizunguma katika mkutano mkuu kwa wanahisa uliofanyika katika matawi yote Nchini Aprili 15 mwaka huu, ambao ulifanyika mwishoni mwa juma lililopita uliowakutanisha kwa ajili ya kusomewa mwenendo wa nenki hiyo kwa mwaka 2011/2012.
Baadhi ya wanahisa wa Benki ya CRDB Wilayani Mbozi, Mkoani mbeya waliohudhuria katika katika mkutano mkuu kwa wanahisa uliofanyika katika matawi yote Nchini Aprili 15 mwaka huu, ambao ulifanyika mwishoni mwa juma lililopita uliowakutanisha kwa ajili ya kusomewa mwenendo wa nenki hiyo kwa mwaka 2011/2012.
******
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Benki ya CRDB, tawi la Wilaya ya Mbozi, Mkoani Mbeya imepiga hatua baada ya kuwa na wateja wengi kwa kipindi cha muda mfupi cha miaka mine tangu ianze kutoa huduma katika wilaya hiyo.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa benki hiyo wa wilaya hiyo Bwana Cornelius Msigwa, katika mkutano mkuu kwa wanahisa uliofanyika katika matawi yote Nchini Aprili 15 mwaka huu, ambao ulifanyika mwishoni mwa juma lililopita uliowakutanisha kwa ajili ya kusomewa mwenendo wa nenki hiyo kwa mwaka 2011/2012.
Meneja huyo aliwashukuru wananchi wote wa wilaya hiyo kwa wito wao wakuwa wateja katika benki hiyo, ambapo mpaka sasa inawateja zaidi ya 7000 na wanahiza wapatao 50 wamekuwa chachu ya kukua kwa tawi hilo.
Bwana Msigwa amesema nia ya kufungua tawi hilo katika wilaya hiyo mwaka 2008, ni kuondokana na usumbufu kwa wateja wao ambao walikuwa wakisafiri umbali mrefu wa zaidi ya kilometa 70, kuifuata huduma yao Jijini Mbeya na hivyo kuhatarisha usalama wao wateja na pesa zao.
Aidha benki hiyo imeboresha huduma zake kwa kutoa huduma za kadi ya ATM na kadi ya JUMBO, ambazo zimeondoa usumbufu wa kupanga foleni na kuokoa muda.
Ameongeza kuwa wateja wanapaswa kurejesha mapema pesa wanazozikopa, ili pesa hizo zitumike kuwakopesha wateja wengine hasa kipindi hiki cha mavuno ya zao la kahawa kinapokaribia na benki hiyo imepania kumkomboa mkulima katika msimu huu.
Kabla ya mkutano huo Afisa wa benki hiyo ambaye ni mwezeshaji wa semina kwa umma katika tawi hilo Bwana Nassib Mwadadi, aliwataka wanahisa kuwa na tabia ya kuwekeza hisa katika benki, kuwa na ufahamu wa hisa nyingine,nafasi ya wanahisa, uatangazaji wa matokeo na ulipaji wa gawio na njia mbalimbali za ulipaji wa hisa.
Katika mkutano huo mbali na kupata taarifa ya mapato na matumizi iliyokaguliwa ilimchagua mjumbe wa kushiriki mkutano mkuu wa benki ya CRDB nchini utakaofanyika June 23 katika Ukumbi wa AICC ambapo Meneja wa tawi hilo Bwana Msigwa alichaguliwa na wanahisa kupitia wingi wa hisa zao.
0 comments:
Post a Comment