Pages


Home » » KUCHELEWA KWA FEDHA YA RUZUKU KUTOKA SERIKALI KUU YA KWAMISHA UTEKEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO MBARALI

KUCHELEWA KWA FEDHA YA RUZUKU KUTOKA SERIKALI KUU YA KWAMISHA UTEKEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO MBARALI

Kamanga na Matukio | 04:36 | 0 comments
Na Kenneth Ngelesi, Mbarali
Ucheleweshaji  wa fedha za ruzuku kutoka Serikali  kuu  inaelezwa kuwa ndiyo kikwazo kikubwa cha utekezaji wa miradi ya mbalimbali ya maendeleo katika wilaya Mbarali Mkoani Mbeya.

Hayo yalibanisha mwishoni mwa juzi na  Mwenyekiti wa Hamashauri ya wilaya ya Mbarali Kenneth Ndingo mjini Rujewa wakati wa kikao  cha baraza la madiwani na   wakuu wa  idara zote kilicho fanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo mjini Rujewa na kuhudhuriwa na mkuu wa wilaya Kanali msaafu Cosmas Kayombo

Katika kikao hicho mwenye kiti huyo alisema licha ya nadiwani kupisha bajeti ya mwaka 2011-2012 kwa ajili ya utekeleza wa miradi mbali mbali lakini imekwama kutekelezwa  kutokana na fedha walizo omba kutoka serikari kuu kutofika kwa wakati.

Akizungmza mbele ya madiwani hao Ndingo alisema kuwa katika bageti ya mwaka huo wa fedha hamashauri ilikusidia kujengamiradi mbalimbali ikiwa ni pamoja miundombinu ya barabara, umwagiliaji, majosho, maramba, shule za msingi na sekondari na ujenzi wa vituo vya afya  pamoja na jingo la utawala la idara ya afya lakini miradi hiyo haukute kelezwa kutokana na tatizo hilo,hata hivyo aliwaambia  madiwani hao kuwa miradi ipo katika hatua za kuanza kutekelezwa.

Aidha katika hatua nyingine madiwani hao waliomba kupewa ufafanuzi juu ya taasisi zinazo toa huduma a ukimwi katika kata hiyo zinztakiwa kuwajibika kwa nani kwani madiwani wamekuwa hawaelewa licha ya NGO hizo kuwa katika kata ambazo wao wanawa wakilisha wananchi.

Madiwani hao walizi lalamikiwa tasisi hizo zimekuwa hazitoi taarifa kwa madiwani ho kwa madi kuwa  zinawajibika kwa wafadhili wanao toa misaada kwa ajili ya ukimwi wilayani humo, katika wilaya hiyo kuna NGO’s  12 zinazo jihusisha na huduma ya ukimwi.

Katika suala la ukimwi baraza la madiwani liliazimia kuwa kila diwani anatakiwa kuwe mwenyekiti wa kamati ya ukimwi katika ngazi ya kata ili kuwa na taarifa kamili juu ya watu  tasisi zinazo toa huduma kwa wagonjwa wa ukimwi na pia kuja watoto wanao someshwa na Tasisi hizo.

‘Unajua mwnyekiti tuna  NGO’S zinazo toa huduma ya UKIMWI katika wilaya yetu yenye kata kumi lakin taasisi hazijawa tayari kushikiana na sisi ndiyo maana inatuwia vigum kwa waheshimiwa madiwani kuwa na taarifa kamili kuusu wagonjwa wa ukimwi pia hata watoto wanao wanao hudumiwa na  tasisi hizo,

‘Kwa hiyo mheshiwa mwenyekiti kuna kila sababu ya kutunga sheria ya kuhakikiasha NGO’S hizi tuna shirikiana nazo ili kuwapa nafasi madiwani kuwa na taarufa kamili juu tatizo hili katika wilaya yetu’ alisikika  moja wa Madiwani hao

Aidha katika hatua nyingene madiwani hao walionyeshwa kusitisjhwa na taarfa ya ujauzito kwa wanafunzi 15 katika shule sekondari Mengele na watuhumiwa kutochukuliwa na hatua za kisheria dhidi yao.

Naye Mkuu wa wilaya alisema aliwa sii wakuu wa idara kutowachukia madiwani hasda pale wanapo utekelezaji wa miradi kwani lengo lao ni kuwa kutaka kuije nga wilaya yao.

Alisema kuwa katika hali ya kaweaida kunaweza kukuwa na msuguano baina ya madiwani na watendaji wa serikari lakini dhamira yao iwe ni moja ya kuijenga Mbarali na sio kwa maslai yao binafsi kwa hiyo kuna kila sababu ya kuwa wavumilivu hasa katika shuguli za maendeleo.

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya Cosmasi Kaombo alisema kuwa kwa ujumla wilaya ya Mbarali haiweza kuwa na tatizo la njaa kwani karibu wilaya zote zinazoizuinguka kuna chakula cha kutosha tatizo la kutokuwa na chakula ni kutokana kuzwa kwa bei ndogo hivyo wafanyabiashra wamekuwa wakisita kupeleka chakuna kutokana na tatizo la bei kutowalipa.
Katika wilaya ya Mbarali kumekuwepo na tatizo la chakula katika baadhi ya vijiji na  kukwamisha shuguli mbalimbali za maendeleo kutokana muda mwingi kutuimia  kutafuta chakula bada ya shughuli za maendeleo.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger