Wanafamilia walionusurika kifo baada ya baada ya kufungiwa ndani ya nyumba na kisha kuchomwa moto, usiku wa saa sita Aprili 14 mwaka huu katika Kitongoji cha Mpakani, Kata ya Nsongwi Mantanji, Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya.
Mashuhuda waliosaidia kuzima na kuiokoa familia iliyonusurika baada ya kufungiwa ndani ya nyumba na kisha kuchomwa moto, usiku wa saa sita Aprili 14 mwaka huu katika Kitongoji cha Mpakani, Kata ya Nsongwi Mantanji, Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya.
*******
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Watu 6 wa familia moja wamenusurika kifo baada ya kufungiwa ndani ya nyumba na kisha kuchomwa moto, usiku wa saa sita Aprili 14 mwaka huu katika Kitongoji cha Mpakani, Kata ya Nsongwi Mantanji, Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya.
Sakata hilo limetokea baada ya kijana aitwaye Benard Andeson (25), ambaye ni jirani wa familia hiyo alipokwenda nyumbani katika nyumba hiyo na kufunga kufuli milango ya nyumba hiyo, huku wakiwa wamelala, kisha kuichoma kwa moto na kutokomea kusiko julikana usiku huo.
Walionusurika katika mkasa huo ni pamoja na mama wa familia hiyo Roza Mwanantwale (51), na watoto wake watano Christina Japhet (20), Sakani Jophet (16), Chesco Jopget (14), Onesmo Japhet (11) na Felister Japhet (4).
Wakati wa tukio hilo baba wa familia hakuwepo nyumbani hapo, ambaye anafahamika kwa jina la Bwana Japhet Mwalizi (55), ambaye yupo Nchi ya Malawi akitafuta riziki.
Baada ya kuchoma moto nyumba hiyo Benard pia alifunga milango ya nyumba zote za majirani kwa kufuli, ili wasitoke kutoa msaada lakini alisahau kufunga nyumba moja ya Bwana Rosa Shabani, ambaye alitoka nje na kupiga yowe hivyo baadhi yao walitoka nje na kwenda kutoa msaada.
Wasamalia hao walivunja mlango na kuinusuru familia hiyo na kuokoa baadhi ya vitu vilivyokuwemo ndani katika nyumba hiyo.
Balozi wa shina katika eneo hilo Bwana Rashid William, amesema alisikia sauti katika nyumba hiyo ndipo walipoenda kutoa msaada lakini, lakini ikawa vigumu kuumudu moto huo ulioteketeza kabisa nyumba hiyo, ambapo walitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mpakani.
Baada ya kutoa taarifa kwa Mwenyekiti huyo walianza kufanya msako usiku huo huo kumsaka Benard na kufanikiwa kumkamata saa 8 usiku, akijaribu kutoroka kuelekea Iwalanje, umbali wa kilometa 20 kutoka kijijini hapo na kumrejesha.
Mtuhumiwa alikiri kutenda kosa hilo majira ya saa nne usiku, na wananchi hao waliamua kumpeleka katika Kituo cha Polisi cha Uyole, kilichopo mkoani hapa.
Hata hivyo wakazi wa mtaa huo waliamua kuchangishana pesa kwa ajili ya kuisaidia familia hiyo, kuezeka upya nyumba yao ambapo shilingi 167,200 zilipatika papo hapo kwaajili ya kununulia mabati na baadhi yao walijitolea miti na misumari, ili familia hiyo iweze kurudi katika nyumba yao kwani hivi sasa wanapatiwa hifadhi na majirani.
Kabla ya kuchoma moto nyumba hiyo mtuhumiwa Benard alitoa vitisho kwa majirani akiwemo Rosa Shaban, ambapo Aprili 11 mwaka huu, alisema kuwa lazima ale maini yake akimaanisha kuwa atamuua na baadae alienda kwa familia hiyo iliyochomewa nyumba, simu moja baada ya tukio na kutoa vitisho kuwa lazima awatoe duniani.
Sababu ya mtuhumiwa kwenda kutoa vitisho hivyo ni kwa madai kuwa kwanini binti wa familia hiyo Christina Josephat amefanikiwa kuhitimu Kidato cha nne, wakati yeye kashindwa kuhitimu shule.
Wakati huo huo Benard Anderson (25) alishindwa kuendelea na masomo ya kitado cha nne katika Shule ya Sekondari Iwalanje, kutokana na utovu wa nidhamu.
0 comments:
Post a Comment