Pages


Home » » AUAWA KWA TUHUMA ZA UCHAWI - MBEYA

AUAWA KWA TUHUMA ZA UCHAWI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:50 | 0 comments
*Atembezwa hadharani akiwa mtupu.
*Akutwa akifukia dawa.
*Akutwa na hirizi mbili na pesa kiunoni.

 Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Wimbi la mauaji Mkoani Mbeya lazidi kupamba moto, Alex Mwang’onda mkazi wa Wakulima eneo la Makunguru ameuawa na vijana wenye hasira kali baada ya kukutwa akiwanga nyumbani kwa Jubel Mbekule, mtaa wa Mkombozi maarufu kwa jina la Kwa Chaula.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 10:30 alfajiri, April 11 mwaka huu ambapo Mzee Alex alikutwa akiwa na hirizi mbili, mizizi inayodaiwa kuwa ni dawa ya kienyeji na pesa taslimu shilingi 2, 000 za kitanzania.

Marehemu aliaga kwa mke wake Bi Amina Alex (42), Aprili 10 mwaka huu majira ya saa 3:00 asubuhi akidai kuwa anakwenda shambani eneo la Kawetele Wilaya ya Mbeya Vijijini lakini toka muda huo hakurudi nyumbani hadi alipokutwa asubuhi akiwa hana nguo ndipo mkewe alitoa vitenge ili kumsitiri mkewe.

Alex ambaye ni Balozi wa shina kwewnye mtaa wake amesema haelewi kilichotokea hadi kukutwa kwenye eneo hilo lililobainishwa na mtoto wa Bwana Mbekule, aitwaye  Adija Mbekule (17), amesema kuwa alikisikia kishindo nje ya nyumba yao na baadae alisikia kama mtu anachimba kitu na kuamua kumwamsha mama yake aitwaye Tausi Rashid.

Baada ya kuamshana wote kwa pamoja walitoka nje na kumkuta Mzee Alex akiwa mtupu na kisha kumuamsha Mwenyekiti wa mtaa Bwana Alfred Mwasumbi, ambaye alimtaka aeleze ametokea wapi  na mtuhumiwa kudai ametokea Makunguru.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa kuna matukio mengi ya kishirikina mtaani kwao hali inayopelekea kuishi kwa wasiwasi alibainisha Balozi wa Mtaa Athanas Mbawa na balozi msaidizi Bi Elizabeth Kapungu.

Hata hivyo vijana wenye hasira kali walimtembeza utupu Mzee huyo hadi nyumbani kwake amakoishi majira ya saa moja asubuhi na kumsababishia umati mkubwa eneo la Soweto kutaharuki huku watoto wakichelewa kwenda shule.

Alipofika nyumbani kwake wananchi walimtoa nje na kuanza kumpiga kwa mapanga na fimbo hatimaye kumwagia mafuta ya taa na kumchomba moto.

Jeshi la Polisi walipewa taarifa na Mwenyekiti wa mtaa lakini walichelewa kufika eneo la tukio, licha ya kupewa taarifa mapema.

Mkuu wa upelelezi mkoani hapa Elias Mwita alisema angetuka askari wake mapema kifuka eneo la tukio lakini alisikitishwa na kitendo cha wananchi kujichukulia sheria mkononi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Bwana Evans Balamaamewalaumu Jeshi la Polisi kwa kutofika mapema eneo la tukio licha ya kupewa taarifa mapema, ambapo walifika majira ya saa mbili asubuhi na kukuta mwili wa marehemu umeanza kuteketea kwa moto, ambapo walimpelewka Hospitali ya Rufaa jijini hapa.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger